Assad: Mashambulizi ya Uingereza si halali
Assad: Mashambulizi ya Uingereza si halali

Rais wa Syria Bashar al-Assad amelaani hatua ya Uingereza kufanya mashambulizi nchini mwake akisema sio halali.
Katika
mahojiano na gazeti la Sunday Times, rais Assad anasema kuwa
mashambulizi ya ndege za kijeshi za Uingereza dhidi ya kundi la
wanamgambo wa Daesh ama Islamic State ni kinyume na maadili ya kimataifa
na inakiuka uhuru wa taifa lake.Bwana Assad anasema mashambulizi hayo yanakoleza na kueneza saratani ya ugaidi.

Assad amesema kuwa mashambulizi ya Urusi yanasaidia kuilinda bara Ulaya.

Majeshi ya Uingereza yalianza kuishambulia Syria siku ya Alhamisi baada ya bunge la taifa hilo kuidhinisha mswada wa kupambana na Islamic state ama Daesh.
No comments:
Post a Comment