LIST YA VIWANJA KUMI NA MBILI VITAKAVYO TUMIKA KOMBE LA DUNIA 2022 QATAR.
Nchini ya Qatar ambaye ndiye mwenyeji wa Michuano ya Kombe la Dunia 2022 mtandao wasokka.com umetoa list pichaz 12 za viwanja vinavyotajwa kuwa vitatumika katika mihuano hiyo 2022. Mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee pichaz 12 za muonekano wa viwanja 12 vilivyotajwa na sokka.com kuwa vitatumika 2022.
1- Lusail Iconic Stadium

Huu upo mji wa Al-Daayen na unamilikiwa na kamati ya Olympic ya Qatar na una uwezo wa kuchukuwa mashabiki 86,250, utattumika katika mechi za makundi ya michuano hiyo, 16 bora, robo fainali, nusu fainali na fainali.
2- Khalifa International stadium

Upo mji wa Al-Rayyan na unamilikiwa na serikali na kamati ya Olympic unauwezo wa kuchukua mashabiki 50000. Utatumika katika mechi za makundi, 16 bora, robo fainali na nusu fainali.
3- Sports City stadium

Utachezewa mechi za makundi na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu upo mji wa Doha na unauwezo wa kuchukua mashabiki 47,560.
4-Al-Khor Stadium

Hiki pia kinamilikiwa na serikali pamoja na Qatar Olympic Committee kipo mji wa Al-Khor kitatumika kuchezea mechi za makundi na 16 bora pia kina uwezo wa kubeba mashabiki 45,330.
5-Al-Shamal Stadium

Huu utachezewa mechi za hatua ya makundi lakini unamilikiwa pia na Serikali ya Qatar pamoja na Qatar Olympic Committee. Upo mji wa Al-Shamal unauwezo wa kuchukua mashabiki 45,120.
6-Al-Wakrah Stadium

Mji wa ambao Al-Wakrah upo uwanja huu utapata nafasi ya kuona mechi za makundi na 16 ya michuano hiyo. Unamilikiwa na Serikali ya Qatar na Qatar Olympic Committee ukiwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 45,120.
7-Umm Slal Stadium

Mji wa Umm Slal utapata nafasi ya kushuhudia mechi za makundi, 16 bora na robo fainali zitakazochezwa katika uwanja huo. unamilikiwa na serikali ya Qatar na unauwezo wa kuchukua mashabiki 45,120.
8-Doha Port Stadium

Mji wa Doha ndio kipo kiwanja hiki kinachomilikiwa na Serikali ya Qatar kitatumika katika mechi za makundi, 16 bora na mechi za robo fainali. kinaripotiwa kuwa na uwezo wa kubeba mashabiki 44,950.
9- Education city stadium

Hiki ni kiwanja kingine kilichopo Al-Rayyan Qatar ambacho kitatumika katika michuano hiyo. Uwezo wake wa kuchukua mashabiki ni 45,350.
10-Al-Gharafa Stadium

Kipo mji wa Al-Rayyan na kitatumika katika mechi za hatua ya makundi pekee. Uwezo wa kuchukua mashabiki ni 21,282.
11-Al-Rayyan Stadium

Hiki ni kiwanja kingine kitakachotumika katika michuano hiyo kipo katika mji wa Al-Rayyan, huu ni uwanka ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 21,282.
12- Qatar University Stadium

Doha kutakuwa na uwanja mwingine utakaotumika katika michuano ya Kombe la Dunia 2022 ukiwa na uwezo wa kubeba mashabiki 43,520.
No comments:
Post a Comment