Friday, April 29, 2016

Mmarekani ahukumiwa kufungwa na kazi ngumu Korea.


KimImage copyrightReuters
Image captionKim alipatikana na makosa ya kufanya ujasusi
Raia wa Marekani amefungwa jela miaka 10 na kazi ngumu nchini Korea Kaskazini baada ya kupatikana na makosa ya kufanya ujasusi, shirika la habari la Uchina la Xinhua limeripoti.
Kim Dong-chul, raia wa Marekani aliyezaliwa Korea Kusini, alikamatwa mwezi Oktoba mwaka jana.
Kim aliwasilishwa kwa wanahabari mjini Pyongyang mwezi jana na akaoneshwa akikiri makosa, na kusema kwamba alilipwa na Korea Kusini kufanya ujasusi.
Mwezi Machi, mwanafunzi mwingine Mmarekani alifungwa jela miaka 15 kwa kujaribu kuiba bango la propaganda.
Alipatikana na makosa ya "uhalifu dhidi ya dola”.
Kim amefungwa jela katika kipindi ambacho uhusiano baina ya Korea Kaskazini na Umoja wa Mataifa, Marekani na nchi nyingine za Magharibi umedorora.
Image copyrightReuters
Majuzi, Pyongyang imefanya msururu wa majaribio ya kurusha makombora baada ya kufanyia majaribio bomu ya nyuklia mwezi Januari, majaribio yote yakivunja vikwazo zilivyowekwa na UN.
Pyongyang ilijaribu kurusha makombora mawili ya masafa ya wastani Alhamisi lakini yalilipuka na kuanguka baharini muda mfupi baada ya kurushwa.
Hatua hiyo ilipelekea kuitishwa kwa mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Serikali mpya ya umoja yaundwa Sudan Kusini.


Image captionMakubaliano ya amani nchini Sudan Kusini
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amelivunja bunge lake na kuunda serikali ya umoja, katika harakati za kupiga jeki makubaliano ya amani yanayolenga kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya takriban miaka miwili.
Mpango huo unaowashirikisha waliokuwa waasi katika serikali ulitangazwa Alhamisi katika runinga ya taifa.
Thuluthi moja ya mawaziri wa bunge hilo jipya ni wanachama wa chama cha SPLM-IO kilichobuniwa na aliyekuwa kiongozi wa waasi Riek Machar,ambaye alirudi mjini Juba mapema wiki hii ili kuapishwa kuwa makamu wa kwanza wa rais.
Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa aliunga mkono hatua hiyo kama ya kihistoria katika makubaliano hayo ya amani.
Makumi ya maelfu wameuawa na watu milioni 2 wakiwachwa bila makao katika mgogoro huo wa Sudan Kusini ambayo ilipata uhuru wake mwaka 2011.

Wednesday, April 27, 2016

TANZANIA YATAJWA KWENYE LIST YA NCHI KUMI DUNIANI AMBAZO UCHUMI WAKE UTAKUA KWA HARAKA.
Image result for TANZANIA
Ripoti ya World Economic Outlook ‘WEO’ ambayo inatoa makadirio ya maendeleo yakiuchumi katika ngazi ya kimataifa, ripoti hiyo hutolewa April na September/October kila mwaka ambapo hutumia database kupata taarifa za akaunti za taifa, mfumuko wa bei, viwango vya ukosefu wa ajira, bei za bidhaa n.k.
Katika ripoti yake ya April 2016 imeitaja nchi ya Myanmar kuwa ndio nchi inayotajwa kuongoza nchi zinazotarajiwa kurejea katika ukuaji mkubwa wa uchumi kwa pato linalokadiriwa kukua kwa 8.6% kwa mwaka.
Ivory Coast imekuwa nchi ya pili na makadirio ya ukuaji wa pato la Taifa la 8.5% mwaka huu. Nchi zingine zilizotabiriwa kurudi takwimu ya juu ya ukuaji ni pamoja na India, Laos na Tanzania.

Benki ya Chase yafunguliwa tena Kenya.


Chase
Image captionWateja wanaruhusiwa kutoa hadi $10,000
Benki ya Chase iliyokuwa imefungwa wiki tatu zilizopita baada ya kukumbwa na matatizo ya kifedha imefunguliwa tena.
Wateja wengi wamefika katika matawi ya benki hiyo kutoa pesa na wengine kutekeleza shughuli nyingine za kibiashara.
Wateja ambao walikuwa wameweka pesa zao katika benki hiyo wanaruhusiwa kutoa hadi shilingi 1milioni ($10,000; $6,800).
Benki ya Chase ndiyo ya tatu kuwekwa chini ya mrasimu nchini Kenya katika kipindi cha miezi sita, hatua iliyozua wasiwasi kuhusu uthabiti wa sekta ya benki nchini Kenya.
Benki nyingine zilizowekwa chini ya mrasimu ni Benki ya Imperial na Benki ya Dubai.
Gavana wa Benki Kuu ya Kenya (CBK) Dkt Patrick Njoroge amepuuzilia mbali wasiwasi kuhusu sekta hiyo na kusema benki hiyo inachukua hatua kudhibiti hali.
Aidha, amewaahidi wateja walioweka amana pesa zao kwenye benki kwamba pesa zao ziko salama.
Benki ya Chase itasimamiwa kwa muda na Benki ya Kenya Commercial (KCB).
Afisa mkuu mtendaji wa KCB Joshua Oigara ameeleza matumaini yake kwamba benki hiyo itajikwamua na kuimarika tena.

Trump ashinda mchujo majimbo matano muhimu.


TrumpImage copyrightAFP
Image captionTrump amesema kwa sasa yeye ni kama "mgombea mteule"
Donald Trump ameshinda mchujo wa kuteua mgombea urais wa chama cha Republican katika majimbo matano ya Marekani yaliyopiga kura Jumanne.
Mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton ameshinda majimbo manne kati ya matano yaliyoshiriki mchujo.
Baada ya matokeo kubainika, Bw Trump alijitangaza kuwa “mgombea mteule” wa Republican.
Ushindi wake Connecticut, Delaware, Maryland, Pennsylvania na Rhode Island unamfanya kukaribia sana kutimiza idadi ya wajumbe inayohitajika kumhakikishia ushindi kabla ya kuandaliwa kwa mkutano mkuu wa chama hicho wa kuidhinisha mgombea Julai.
Upande wa Democratic, Bi Clinton amenyimwa ushindi kamili na Bernie Sanders ambaye ameshinda katika jimbo la Rhode Island.
Bw Sanders ameaoa kuendelea na mchujo.
ClintonImage copyrightReuters
Image captionBi Clinton amesema kampeni yake ina "malengo jasiri"
Akiongea katika ukumbi wa mikutano wa Philadelphia baada ya kushinda majimbo hayo manne, Bi Clinton amesema kampeni yake inaweka “malengo jasiri na ya kupiga hatua mbele” katika kuimarisha maisha ya watu Marekani.
“Sisi tunaamini katika wema wa watu wetu na ukuu wa taifa letu,” alisema.
Naye Bw Trump aliwaambia wafuasi wake New York kwamba hatabadilisha sera zake iwapo atachaguliwa kuwa rais.
"Sibadiliki,” alisema. “Mnafahamu kwamba nilisomea shule bora zaidi. Mimi ni mtu mwerevu sana. Nitaiwakilisha nchi hii kwa heshima na vyema sana.
"Lakini sitaki kubadilisha sifa zangu binafsi. Mnajua, ndizo zilizonifikisha hapa.”
Wapinzani wake, Ted Cruz na John Kasich, tayari wameanza kuangazia majimbo yajayo, wakiungana kusaidiana kushinda majimbo ya Indiana, Oregon na New Mexico.
Bw Trump ameshutumu ushirika wao akisema ni ishara ya kukata tamaa.

Tuesday, April 26, 2016

WANA CLUB YA LIBRARY AND INFORMATION MANAGEMENT WAKIENDESHA MDAHARO KUHU...

Ukilala katika kitanda kipya hutalala vyema


Image copyrightThinkstock
Image captionUkilala katika kitanda kipya hutalala vyema
Je ushawahi kugundua kuwa ukilala katika kitanda au mazingira mapya haupati usingizi wa kutosha?
Sasa basi, Utafiti umebaini kuwa mtu akilala katika mazingira mapya ubongo wake haulali wote!
Upande wa kushoto wa ubongo huwa uko chonjo dhidi ya hatari yeyote ile, hivyo haulali.
Utafiti huo wa chuo kikuu cha Brown ulioongozwa na Profesa Yuka Sasaki,sasa umeanza kujaribu kutegua kitendawili cha iwapo mtu anaweza kuzima upande wake wa kushoto wa ubongo anapolala katika mazingira mapya?
Picha za ubongo wa watu waliojitolea katika utafiti huu zinaonesha kuwa upande huo wa kushoto huwa ukitahadhari endapo patatokea sauti yeyote itakayoashiria hatari.
Utafiti huu ulithibitishwa vilevile katika ndege na wanyama wengine.
Image captionUpande wa kushoto wa ubongo huwa uko chonjo dhidi ya hatari yeyote ile, hivyo haulali.
Utafiti mbadala katika chuo kikuu cha Rhode Island umeonesha kuwa ubongo wa binadamu unaweza kubadilika kadri inavyokabiliwa na changamoto mpya.
Aidha Mtafiti huyo Sasaki anasema kuwa dhihirisho la hilo linapatikana kwa watu wanaosafiri kila kukicha.
''Siamini kuwa mtu ambaye analala katika mazingira mapya kila kukicha atakosa usingizi,bila shaka itafikia wakati ambapo atalala tu usingizi wa pono''

Lucy Kibaki afariki.


Image captionLucy kibaki na mkewe wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2007
Mke wa kwanza wa rais Lucy Kibaki amefariki katika hospitali mmoja mjini London kwa ugonjwa usiojulikana.
Lucy alipata umaarufu kwa kumchapa kofi mpiga picha mmoja mwaka 2005 wakati alipovamia afisi za kituo kimoja cha habari mwaka 2005 akikasirishwa na vile habari moja ilivyoandikwa.
Katika kumbukumbu ya kumuhenzi bi Kibaki rais wa Kewnya Uhuru Kenyatta alimsifu kwa jukumu lake kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi nchini Kenya.
Image captionLucy Kibaki pamoja na aliyekuwa mke wa aliyekuwa rais wa Marekani George Bush ,Laura Bush.Picha kwa niaba ya Getty Images
Bwana Kenyatta alimrithi mumewe bwana Kibaki ambaye alitawala kutoka mwaka 2002 hadi 2013.
Bi Kibaki aliyezaliwa mwaka 1940,alijiondoa katika maisha ya hadharani wakati wa mwisho wa utawala wa mumewe.
Image captionLucy Kibaki na mumewe Mwai KIbaki wakiwapungia mkono wafuasi wao mda mchache baada ya kibaki kuwasilisha stakhabadhi zake za uchaguzi katika tume ya uchaguzi mwaka 2007.Picha ni kwa niaba ya Getty images
Mara ya mwisho kuonekana hadharani ni mwezi Agosti mwaka 2010,wakati alipofurahishwa na kupatikana kwa katiba mpya.
Image captionLucy Kibaki na mumewe aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki pamoja na mkewe marehemu Kijana Wamalwa wakati wa misa ya kifo cha Wamalwa.Picha kwa niaba ya Getty Images
Bwana Kenyatta alisema kuwa alikuwa mgonjwa kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita ambapo amekuwa akipata matibabu nchini Kenya na Uingereza.Bi Kibaki ni mwalimu ambaye aliwacha kazi yake kabla ya ndoa yake na kibaki mwaka 1962 ili kuwalea wanawe.

Machar aapishwa kuwa makamu wa rais Sudan Kusini.


Image captionRiek Machar
Aliyekuwa kiongozi wa waasi Riek Machar ameapishwa kuwa makamu wa rais wa kwanza nchini Sudan Kusini katika serikali mpya ya umoja.
Riek Machar ameapishwa mda mfupi baada ya kuwaasili katika mji mkuu wa Juba ,baada ya kuchelewa kwa kipindi cha juma moja hatua iliohatarisha kuanguka kwa makubaliano ya amani nchini humo.
Hiyo ni hatua muhimu ya makubaliano yanayolenga kumaliza mgogoro wa zaidi wa miaka miwili ambao umesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya raia huku takriban watu milioni mbili wakiwachwa bila makao.
Bw Machar aliutoroka mji wa Juba wakati wa kuanza kwa mgogoro huo mnamo mwezi Disemba mwaka 2013.
MacharImage copyrightReuters
Image captionBw Machar amesema changamoto kubwa ni kuhakikisha mkataba wa kusitisha mapigano unatekelezwa kote nchini humo
Ametuhumiwa kwa kujaribu kupanga mapinduzi ambayo anakana ,lakini yalisababisha mauaji ya kulipiza kisasi ambayo yalipelekea kuwepo kwa mgogoro huo.
Kundi lake linasema kuwa kuchelewa huko kulisababishwa na mipango ya serikali na kwamba aikuwa amepanga kurudi siku ya Jumatano.
Taarifa kutoka kwa serikali siku ya Jumanne ilikuwa imesema kuwa kurejea kwa Machar kulicheleweshwa kwa kutaka kuwasili mjini Juba akiwa na silaha kali.

Monday, April 18, 2016


Watu zaidi  ya  270  wamekufa  kutokana  na  tetemeko la ardhi nchini Ecuador. Na wengine zaidi ya 2000  wamejeruhiwa. Tetemeko hilo lililofikia nguvu  ya 7.8  ya kipimo cha Richter liliikumba nchi hiyo  Jumamosi na kusababisha  madhara makubwa. Majengo mengi yalianguka na kuwafukia watu. Ingawa janga  hilo la asili lilichukua muda  wa  dakika  tano tu lilikuwa baya kabisa kuwahi kuikumba Ecuador katika muda  wa miaka 40 iliyopita. 
Wakati huo huo wafungwa  wapatao 100 walitoroka jela baada ya tetemeko hilo kutokea. Lakini  waziri  wa sheria  alifahamisha katika mtandao  wa  kijamii wa  twitter kwamba wafungwa 30  wamekamatwa tena katika  jimbo la Manabi magharibi  mwa  Ecuador.  

Watu 250,000 watakiwa kuhama makwao Japan.


TetemekoImage copyrightAP
Image captionTetemeko la kwanza lilitokea Alhamisi wiki iliyopita
Watu karibu 250,000 wametakiwa wahame kutokana na wasiwasi wa kutokea kwa mitetemeko zaidi ya ardhi nchini Japan, shirika la kutoa misaa limesema.
Naoki Kokoawai, mshauri wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Japan, ameambia BBC kwamba makundi zaidi ya matabibu yanatumwa maeneo ya kusaidia waathiriwa.
Mitetemeko miwili mikubwa ilitikisa kisiwa cha kusini magharibi cha Kyushu wiki iliyopita na kuua watu 42.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa imetahadharisha kwamba kuna uwezekano mkubwa wa mitetemeko zaidi huenda kutokea siku chache zijazo.
Image copyrightEPA
Watu zaidi ya 1,000 walijeruhiwa na miundo mbinu mingi kuharibiwa.
Wafanyakazi karibu 30,000 wa uokoaji wanasaidia kutafuta manusura. Polisi wamesema watu 11 bado hawajulikani walipo, kwa mujibu wa shirika la utangazaji la serikali la NHK.
"Bado kuna watu ambao hawajulikani walipo. Tunataka kufanya juhudi zaidi na kuwaokoa watu,” Waziri Mkuu Shinzo Abe aliambia Bunge mapema Jumatatu.
Amesema anataka kutangaza eneo lililoathiriwa kuwa eneo la janga.
NyumbaImage copyrightAFP
Image captionNyumba nyingi zimebomoka
Mwanamke wa umri wa miaka 61 alipatikana akiwa amefariki karibu na nyumba yake iliyoporomoka eneo la Kumamoto mnamo Jumapili, gazeti la Japan Times liliripoti.
Tetemeko la ardhi la nguvu ya 7.3 lilitokea karibu na jiji la Kumamoto, ambalo lilikuwa limeathiriwa na tetemeko jingine la nguvu ya 6.4 Alhamisi usiku.
Mitetemeko hiyo miwili ilisababisha uharibifu mkubwa.
Jeshi la Marekani limesema liko tayari kutoa usaidizi wa ndege kusaidia juhudi za uokoaji.