Rais Deby anatarajiwa kushinda uchaguzi wa Chad.
Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Chad baada ya uchaguzi wa hapo jana unaotarajiwa kumpa ushindi Rais Idriss Deby na kuurefusha utawala wake wa miaka 26 madarakani. Deby alipambana na wapinzani 13 lakini anatarajiwa kushinda muhula wa tano baada ya kujiimarisha madarakani katika taifa hilo la Afrika ya Kati. Kiongozi wa upinzani Saleh Kebzabo anahoji kuwa nchi hiyo inahitaji mabadiliko ya uongozi. Chad inasalia kuwa mshirika wa kijeshi wa mtawala wake wa kikoloni Ufaransa. Matokeo yanatarajiwa baada ya wiki mbili, kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na tume ya uchaguzi. Katiba ya Chad inamruhusu Deby kugombea lakini alikuwa ameahidi kuurejesha ukomo wa mihula ambao ulifutiliwa mbali na serikali yake mwaka wa 2004. Viongozi wengine wa Afrika wamekuwa wakijaribu kufuta ukomo wa mihula ili kurefusha uongozi wao madarakani, na kusababisha machafuko nchini Burundi, Burkina Faso na Jamhuri ya Congo.
No comments:
Post a Comment