Tuesday, April 26, 2016

Machar aapishwa kuwa makamu wa rais Sudan Kusini.


Image captionRiek Machar
Aliyekuwa kiongozi wa waasi Riek Machar ameapishwa kuwa makamu wa rais wa kwanza nchini Sudan Kusini katika serikali mpya ya umoja.
Riek Machar ameapishwa mda mfupi baada ya kuwaasili katika mji mkuu wa Juba ,baada ya kuchelewa kwa kipindi cha juma moja hatua iliohatarisha kuanguka kwa makubaliano ya amani nchini humo.
Hiyo ni hatua muhimu ya makubaliano yanayolenga kumaliza mgogoro wa zaidi wa miaka miwili ambao umesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya raia huku takriban watu milioni mbili wakiwachwa bila makao.
Bw Machar aliutoroka mji wa Juba wakati wa kuanza kwa mgogoro huo mnamo mwezi Disemba mwaka 2013.
MacharImage copyrightReuters
Image captionBw Machar amesema changamoto kubwa ni kuhakikisha mkataba wa kusitisha mapigano unatekelezwa kote nchini humo
Ametuhumiwa kwa kujaribu kupanga mapinduzi ambayo anakana ,lakini yalisababisha mauaji ya kulipiza kisasi ambayo yalipelekea kuwepo kwa mgogoro huo.
Kundi lake linasema kuwa kuchelewa huko kulisababishwa na mipango ya serikali na kwamba aikuwa amepanga kurudi siku ya Jumatano.
Taarifa kutoka kwa serikali siku ya Jumanne ilikuwa imesema kuwa kurejea kwa Machar kulicheleweshwa kwa kutaka kuwasili mjini Juba akiwa na silaha kali.

No comments:

Post a Comment