Nchi wazalishaji wa mafuta duniani kukutana Qatar hii leo.
Wawakilishi wa nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi duniani wanatarajiwa kukutana nchini Qatar hii leo ili kufikiria uwezekano wa kupunguza uzalishaji wa bidhaa hiyo. Kuporomoka kwa bei ya mafuta kumeathiri uchumi wa nchi zenye utajiri wa mafuta hususani Nigeria, Venezuela na Urusi. Maafisa kutoka mataifa hayo hivi sasa wanaandaa mpango utakaowezesha kupunguza uzalishaji wa mafuta hali ambayo inaweza ikasababisha kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo. Saudi Arabia ambayo ni nchi inayoongoza kuzalisha mafuta kwa wingi duniani imesema itakubaliana na hatua ya kupunguza uzalishaji huo iwapo Iran nayo itakubali kufanya hivyo. Hata hivyo serikali ya Iran inaonekana kutokubaliana na mpango huo na inakusudia kususia kikao hicho cha leo nchini Qatar. Hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa shirika la habari la Iran- SHANA.
No comments:
Post a Comment