Tuesday, April 26, 2016

Ukilala katika kitanda kipya hutalala vyema


Image copyrightThinkstock
Image captionUkilala katika kitanda kipya hutalala vyema
Je ushawahi kugundua kuwa ukilala katika kitanda au mazingira mapya haupati usingizi wa kutosha?
Sasa basi, Utafiti umebaini kuwa mtu akilala katika mazingira mapya ubongo wake haulali wote!
Upande wa kushoto wa ubongo huwa uko chonjo dhidi ya hatari yeyote ile, hivyo haulali.
Utafiti huo wa chuo kikuu cha Brown ulioongozwa na Profesa Yuka Sasaki,sasa umeanza kujaribu kutegua kitendawili cha iwapo mtu anaweza kuzima upande wake wa kushoto wa ubongo anapolala katika mazingira mapya?
Picha za ubongo wa watu waliojitolea katika utafiti huu zinaonesha kuwa upande huo wa kushoto huwa ukitahadhari endapo patatokea sauti yeyote itakayoashiria hatari.
Utafiti huu ulithibitishwa vilevile katika ndege na wanyama wengine.
Image captionUpande wa kushoto wa ubongo huwa uko chonjo dhidi ya hatari yeyote ile, hivyo haulali.
Utafiti mbadala katika chuo kikuu cha Rhode Island umeonesha kuwa ubongo wa binadamu unaweza kubadilika kadri inavyokabiliwa na changamoto mpya.
Aidha Mtafiti huyo Sasaki anasema kuwa dhihirisho la hilo linapatikana kwa watu wanaosafiri kila kukicha.
''Siamini kuwa mtu ambaye analala katika mazingira mapya kila kukicha atakosa usingizi,bila shaka itafikia wakati ambapo atalala tu usingizi wa pono''

No comments:

Post a Comment