IS yateka nyara wafanyakazi 300 wa kiwanda cha saruji
Kundi linalojiita dola la Kiisalmu IS, linashutumiwa kuwateka nyara zaidi ya wafanyakazi 300 wa kiwanda cha kuzalisha saruji nchini Syria cha Al-Badia. Kundi hilo lilivamia mji wa Dmeir mashariki mwa mji mkuu wa Damascus, baada ya kupoteza maeneo kadhaa katika mapambano na vikosi vya serikali ya Syria wiki za hivi karibuni, ikiwamo mji wa kihistoria wa Palmyra. Aidha wakaazi wa mji wa Dmeir wamesema zaidi ya watu 250 wote wakiwa ni wafanyakazi wa kiwanda hicho, hawajulikani walipo tokea Jumatatu iliyopita. Haya yanajiri wakati ambapo duru mpya ya mazungumzo ya amani ikitarajiwa kuanza wiki ijayo mjini Geneva, kufuatia usitishwaji wa mapigano baina ya vikosi vya serikali na makundi ya waasi, hatua iliyotowa nafasi kwa serikali kulilenga zaidi kundi la IS.
No comments:
Post a Comment