Watu zaidi ya 270 wafa kutokana tetemeko la ardhi Ecuador'
Watu zaidi ya 270 wamekufa kutokana na tetemeko la ardhi nchini Ecuador. Na wengine zaidi ya 2000 wamejeruhiwa. Tetemeko hilo lililofikia nguvu ya 7.8 ya kipimo cha Richter liliikumba nchi hiyo Jumamosi na kusababisha madhara makubwa. Majengo mengi yalianguka na kuwafukia watu. Ingawa janga hilo la asili lilichukua muda wa dakika tano tu lilikuwa baya kabisa kuwahi kuikumba Ecuador katika muda wa miaka 40 iliyopita.
Wakati huo huo wafungwa wapatao 100 walitoroka jela baada ya tetemeko hilo kutokea. Lakini waziri wa sheria alifahamisha katika mtandao wa kijamii wa twitter kwamba wafungwa 30 wamekamatwa tena katika jimbo la Manabi magharibi mwa Ecuador.
No comments:
Post a Comment