Monday, April 11, 2016

Darfur kupiga kura ya maoni leo.


Image captionDarfur kupiga kura ya maoni leo kuhusu idadi ya majimbo
Jimbo la magharibi mwa Sudan, Darfur linapiga kura ya maoni, miaka 13 baada ya kuanza kwa mzozo wa wenyewe kwa wenyewe uliosababisha watu 300,000 kupoteza maisha.
Kura ya maoni itaamua kama Darfur itakuwa na majimbo matano au jimbo moja, ambapo raia watakuwa na siku mpaka ya jumatano kuamua.
Kura hii inapigwa wakati kukiwa na hali duni ya usalama na watu wengi hawajajiandikisha kupiga kura.
Marekani imeeleza hofu yake kuwa kura hiyo haitakuwa ya haki, lakini Rais Omar al-Bashir amesisitiza kuwa itakuwa huru na haki.
Kura ya maoni ni hatua ya mwisho ya mchakato wa kuleta amani ambayo makubaliano yake yalitiwa saini mjini Doha kwa kipindi kirefu waasi wamekuwa wakiomba kuwepo na mamlaka kwenye miji ili kuzuia kile wanachodai kuingilia kwa mamlaka ya Khartoum kwenye mizozo ya umiliki wa ardhi

No comments:

Post a Comment