Monday, April 18, 2016

Watu 250,000 watakiwa kuhama makwao Japan.


TetemekoImage copyrightAP
Image captionTetemeko la kwanza lilitokea Alhamisi wiki iliyopita
Watu karibu 250,000 wametakiwa wahame kutokana na wasiwasi wa kutokea kwa mitetemeko zaidi ya ardhi nchini Japan, shirika la kutoa misaa limesema.
Naoki Kokoawai, mshauri wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Japan, ameambia BBC kwamba makundi zaidi ya matabibu yanatumwa maeneo ya kusaidia waathiriwa.
Mitetemeko miwili mikubwa ilitikisa kisiwa cha kusini magharibi cha Kyushu wiki iliyopita na kuua watu 42.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa imetahadharisha kwamba kuna uwezekano mkubwa wa mitetemeko zaidi huenda kutokea siku chache zijazo.
Image copyrightEPA
Watu zaidi ya 1,000 walijeruhiwa na miundo mbinu mingi kuharibiwa.
Wafanyakazi karibu 30,000 wa uokoaji wanasaidia kutafuta manusura. Polisi wamesema watu 11 bado hawajulikani walipo, kwa mujibu wa shirika la utangazaji la serikali la NHK.
"Bado kuna watu ambao hawajulikani walipo. Tunataka kufanya juhudi zaidi na kuwaokoa watu,” Waziri Mkuu Shinzo Abe aliambia Bunge mapema Jumatatu.
Amesema anataka kutangaza eneo lililoathiriwa kuwa eneo la janga.
NyumbaImage copyrightAFP
Image captionNyumba nyingi zimebomoka
Mwanamke wa umri wa miaka 61 alipatikana akiwa amefariki karibu na nyumba yake iliyoporomoka eneo la Kumamoto mnamo Jumapili, gazeti la Japan Times liliripoti.
Tetemeko la ardhi la nguvu ya 7.3 lilitokea karibu na jiji la Kumamoto, ambalo lilikuwa limeathiriwa na tetemeko jingine la nguvu ya 6.4 Alhamisi usiku.
Mitetemeko hiyo miwili ilisababisha uharibifu mkubwa.
Jeshi la Marekani limesema liko tayari kutoa usaidizi wa ndege kusaidia juhudi za uokoaji.

No comments:

Post a Comment