Wednesday, April 27, 2016

Benki ya Chase yafunguliwa tena Kenya.


Chase
Image captionWateja wanaruhusiwa kutoa hadi $10,000
Benki ya Chase iliyokuwa imefungwa wiki tatu zilizopita baada ya kukumbwa na matatizo ya kifedha imefunguliwa tena.
Wateja wengi wamefika katika matawi ya benki hiyo kutoa pesa na wengine kutekeleza shughuli nyingine za kibiashara.
Wateja ambao walikuwa wameweka pesa zao katika benki hiyo wanaruhusiwa kutoa hadi shilingi 1milioni ($10,000; $6,800).
Benki ya Chase ndiyo ya tatu kuwekwa chini ya mrasimu nchini Kenya katika kipindi cha miezi sita, hatua iliyozua wasiwasi kuhusu uthabiti wa sekta ya benki nchini Kenya.
Benki nyingine zilizowekwa chini ya mrasimu ni Benki ya Imperial na Benki ya Dubai.
Gavana wa Benki Kuu ya Kenya (CBK) Dkt Patrick Njoroge amepuuzilia mbali wasiwasi kuhusu sekta hiyo na kusema benki hiyo inachukua hatua kudhibiti hali.
Aidha, amewaahidi wateja walioweka amana pesa zao kwenye benki kwamba pesa zao ziko salama.
Benki ya Chase itasimamiwa kwa muda na Benki ya Kenya Commercial (KCB).
Afisa mkuu mtendaji wa KCB Joshua Oigara ameeleza matumaini yake kwamba benki hiyo itajikwamua na kuimarika tena.

No comments:

Post a Comment