Friday, April 8, 2016

Image result for MUGABE
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema watu wanaotaka kumrithi wadhifa wake wa Urais wanamuombea kifo na amewataka wafuasi wa chama tawala cha ZANU-PF washikamane dhidi ya maadui wa nchi za kigeni wanaotaka kuliharibu taifa hilo la Kusini mwa bara la Afrika.
Katika mkutano na wanajeshi wastaafu waliopigana katika  vita  vya uhuru vya miaka ya sabini, Mugabe amesema safari zake za mara kwa mara za nchini Malaysia na Singapore zimepelekea magazeti kuchapisha habari za uwongo kuwa ni mgonjwa anayekaribia mauti, na kusababisha mvutano ndani ya chama chake cha ZANU-PF. Kiongozi huyo mkongwe barani Afrika mwenye umri wa miaka 92, aliingia madarakani mwaka 1980 baada ya nchi hiyo kupata uhuru wake kutoka Uingereza. Aidha Mugabe amesema atakaempokea wadhifa wa urais atachaguliwa kwa njia za kidemokrasia na nafasi hiyo alisisitiza haitorithiwa na mke wake kama inavyovumishwa.

No comments:

Post a Comment