Rais Kenyata awaongoza maelefu ya wakenya kusherehekea kufutiwa mashitaka na ICC.
Rais Uhuru Kenyata wa Kenya hapo jana amewaongoza maelfu ya raia wa nchi hiyo katika mkutano wa hadhara kusherehekea hatua ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya ICC kufuta mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu yaliyokuwa yakimkabili yeye , makamu wake William Ruto pamoja na maafisa kadhaa nchini humo. Mkutano huo ulionekana kupingwa na kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga pamoja na baadhi ya asasi za kiraia kutokana na kile walichodai kuwa ni kuonyesha kutojali machungu waliyo nayo wahanga wa machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo zaidi ya watu 1,000 waliuawa huku wengine 600,000 wakilazimika kuyahama makazi yao. Rais Kenyata na Makamu wake William Ruto ambao walikuwa katika pande mbili tofauti wakati wa machafuko hayo wamesema kuungana kwao ni uthibitisho wa kupunguza mvutano uliopo wa kisiasa na kikabila nchini humo. Mwanzoni mwa mwezi huu mahakama ya ICC ilimfutia mashitaka makamu huyo wa Rais wa Kenya pamoja na mwandishi wa habari nchini humo Joshua Arap Sang kwa maelezo ya kukosekana ushahidi wa kuwatia hatiani wakati mashitaka dhidi ya Rais Kenyata yalifutwa mwezi Desemba mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment