Thursday, March 31, 2016

Waziri wa Rwanda afia gerezani Burundi


Image copyrightGetty
Image captionMiongoni mwa vurugu zilizotokea mji mkuu wa Bujumbura
Waziri wa zamani wa Rwanda Jacques Bihozagara amefariki katika gereza moja nchini Burundi miezi minne baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya ujasusi.
Rwanda imesema marehemu Jacques alikuwa ameshikiliwa kinyume cha sheria.
Balozi wa Rwanda nchini Ubelgiji ameandika na kusema kifo cha Jacques ni "mauaji".
Wafungwa katika gereza alipokuwa ameshikiliwa wanasema alionekana akiwa katika hali nzuri na kwamba alifariki dakika chache baada ya kuchukuliwa kutoka gereza kupelekwa hospitali baada ya kuugua.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukiishutumu Rwanda kwa kujaribu kuipindua serikali ya Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, madai ambayo Rwanda imekuwa ikiyakanusha.

Wafadhili wasitisha misaada kwa Tanzania


Image copyrightStatehouse Tanzania
Image captionRais wa Tanzania John Magufuli.
Kundi la watoa misaada 10 kutoka nchi za magharibi wametangaza kusitisha ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania.
Hii inafuatia uamuzi wa shirika la utoaji misaada la serikali ya marekani kuondoa msaada wa dola 472 wa kufadhili miradi ya maendeleo kutokana na jinsi uchaguzi wa kisiwa cha Zanzibar ulivyoendeshwa.
Karibu theluthi moja ya bajeti ya Tanzania ilitegemea msaada mwaka uliopita, kwa hivyo hatua hizo za hivi punde ni pigo kwa mipango ya maendeleo ya serikali mpya.

Watu wasiopungua 10 wameuawa katika mji wa mashariki mwa India wa Kolkata leo na wengine 150 wanahofiwa kukwama baada ya kuporomoka kwa njia ya juu iliyokuwa inajengwa na kuangukia magari yanayotembea kwenye barabara ya chini. Polisi imesema asakri wa zimamoto pamoja na wakaazo walikuwa wanajaribu kuwaokoa watu waliofunikwa na vifusi vya njia hiyo iliyoporomoka. Afisa wa polisi Raichand Mohta, amesema hali ni mbaya na kwa wakati hakuna anaejuwa ni watu wangapi wamekwama. Njia hiyo hiyo ya juu imekuwa ikijengwa tangu mwaka 2009 na imekuwa ikikosa muda wake wa kukamilishwa kwa mara kadhaa. Miradi ya ujenzi nchini India huwa inakumbwa na ukosefu wa viwango vya usalama.

Image result for IS
Shambulizi lililofanywa na ndege isiyokuwa na rubani karibu na eneo linalodhibitiwa na kundi la kigaidi la dola la kiislamu Raqa limesababisha kifo cha kamanda wa kundi hilo la jihadi aliyekuwa akielekea mkoa wa Aleppo kutokana na maelezo ya mkuu wa kundi hilo.Taarifa hizo zimetolewa leo na kundi linalofuatilia hali ya Syria.Kifo cha kamanda huyo ni tukio la karibuni kabisa kati ya msururu wa matukio ya kushambuliwa kwa kundi hilo la jihadi katika kipindi cha wiki za hivi karibuni na limekuja siku kadhaa baada ya vikosi vya serikali vinavyosaidiwa na Urusi kuudhibiti tena mji wa kale wa Palmyra.Kamanda huyo wa ngazi ya juu wa IS  Abu al-Hija raia wa Tunisia  aliuwawa jana usiku katika shambulio la ndege isiyokuwa na rubani iliyoongozwa na kikosi kinachosimamiwa na Marekani,limesema shirika linalofuatilia haki za binadamu nchini Syria lenye makao yake London.Aidha shirika hilo limesema kamanda huyo alisafiri kwenda Syria  kutoka Iraq kwa maagizo ya kiongozi wa IS Abu Bakr al Baghadadi, katika kipindi cha masaa 24 kabla ya kifo chake.

Mahakama yatupilia mbali kesi Uganda


Image copyright
Image captionRais Yoweri Museveni alitangazwa mshindi
Mahakama ya juu zaidi nchini Uganda imefutilia mbali kesi iliyokuwa ikipinga ushindi wa rais Yoweri Museveni katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi uliopita.
Mahakama hiyo ilisema kuwa licha ya kuwepo kwa dosari nyingi za uchaguzi, matokeo ya mwisho hayakuathiriwa.
Kesi hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo amama mbabazi ambaye alimaliza katika nafasi ya tatu.
Image copyrightAP
Image captionKizza Besigye angali anatumikia kifungo cha nyumbani
Kizza Besigye ambaye alimaliza wa pili amesema hakupata nafasi ya kuwasilisha kesi hiyo mahakamani kwa sababu angali anatumikia kifungo cha nyumbani.
Waangalizi wa kitaifa na kimataifa walishutumu uchaguzi huo ambao ulishindwa na rais Museveni.

Chama chatisha kumuondoa Zuma madarakani


Image copyright
Image captionRais Jacob Zuma
Chama cha Democtratic Alliance nchini Afrika Kusini kumeanzisha kampeni ya kumuondoa rais Jacob Zuma madarakani baada ya mahakama ya kikatiba kutoa uamuzi kuwa alikiuka katiba.
Mahakama ilipata kuwa bwana Zuma alikataa kutii agizo kutoka kwa ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu mwaka 2014 la kamtaka alipe pesa zilizotumika kuifanyia ukarabati nyumba yake ya kibinafsi.
Image copyrightGetty
Image captionNyumba ya Zuma ya Nkandla
Vyama viwili vya upinzani viliwasilisha kesi hiyo mahakamani ili kumlazimu rais Jacob Zuma kuzingatia matokeo ya uchunguzi yaliofanywa na mkaguzi wa hesabu za serikali, kwamba alihusika na mabadiliko yaliofanyiwa nyumba yake ya Nkandla.
Mamilioni ya madola yalitumika katika kile kilitajwa na serikali kuwa uimarishaji wa usalama. Marekebisho hayo yalishirikisha ukumbi,kidimbwi cha kuogelea na zizi la ngombe

Tuesday, March 29, 2016

Jukwaa laanguka Odinga akihutubu pwani ya Kenya.


MalindiImage copyrightAFP
Image captionBw Odinga alikuwa akihutubu mjini Malindi
Video inayoonesha kiongozi wa upinzani Kenya Bw Raila Odinga na viongozi wengine wakianguka baada ya jukwaa kuporomoka akihutubia mkutano wa hadhara imevuma sana mtandaoni Kenya.
Bw Odinga alikuwa akihutubu katika uwanja wa Karisa Maitha mjini Malindi, jimbo la Kilifi katika pwani ya Kenya Alhamisi wiki iliyopita jukwaa lilipodondoka.
Mkutano huo ulikuwa wa kuwashukuru wapiga kura kwa kumpigia kura mgombea wa chama chake cha ODM Willy Mtengo kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika Machi 7.
Bw Mtengo alishinda uchaguzi huo.
Ilikuwa siku moja kabla ya Ijumaa Kuu na Bw Odinga alikuwa akisimulia kuhusu mateso aliyopitia Yesu Kristo.
“Wakati huu mimi nilikuwa nimeenda kule Jericho, nikaonyeshwa ile mlima ya majaribio. Pale ambapo shetani alimpeleka Yesu akamuonesha ulimwengu wote. Akamwambia angalia hii yote. Ukikubali kusujudu na kuniabudu hii yote itakuwa ni yako. Lakini Yesu akamwambia wewe nenda mbali shetani ..” alisema Bw Odinga kabla ya jukwaa kuanguka.
Video hiyo imesambazwa sana mtandaoni.
Bw Odinga alikuwa ziarani Israel mapema mwezi huu.
Naibu mwenyekiti wa chama cha ODM eneo la Kilifi amenukuliwa na gazeti la Daily Nation la Kenya akisema hakuna aliyejeruhiwa kwenye kisa hicho.
Anasema watu waliokuwa kwenye jukwaa walipunguzwa na Bw Odinga akaendelea kuhutubia mkutano huo.

Uchaguzi wa Zanzibar waikosesha hela Tanzania.


Uchaguzi
Image captionMwanamke akipiga kura wakati wa uchaguzi Zanzibar
Shirika la ufadhili la serikali ya Marekani limesitisha msaada wake kwa serikali ya Tanzania likilalamikia matukio kuhusu uchaguzi wa Zanzibar na kutekelezwa kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao.
Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) imesema Tanzania haijatimiza viwango vinavyohitajika ili kunufaika na ufadhili kutoka kwa shirika hilo, na hivyo basi haitapokea msaada wa awamu ya pili ambao ulikuwa wa jumla ya Dola 472.8 milioni ambazo ni sawa na shilingi trilioni moja za Tanzania.
Kupitia taarifa, bodi hiyo imesema: "Serikali ya Tanzania haijachukua hatua za kuhakikisha kuheshimiwa kwa uhuru wa kujieleza na uhuru wa kujumuika katika utekelezwaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao.”
Bodi hiyo aidha imesema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao "haukushirikisha wote na wala haukuakisi maoni ya wote, licha ya malalamiko kutoka kwa serikali ya Marekani na jamii ya kimataifa.”
Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Ali Mohammed Shein alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani, Chama cha Wananchi (CUF).
MCC imesema kwamba huwa inatilia mkazo sana demokrasia na kujitolea kwa nchi kufanikisha uchaguzi huru na wa haki.
"Uchaguzi uliofanyika Zanzibar na kutekelezwa nwa Sheria ya Uhalifu wa Mitandao vinaenda kinyume na hili,” imesema.
Tanzania ilipokea Dola 698 milioni katika awamu ya kwanza.
Pesa za MCC hutumiwa kufadhili miradi ya maji, barabara na nishati.

Image result for UMOJA WA ULAYA
Umoja wa Ulaya unapanga kuiondolea Burundi msaada wa fedha za kusimamia kikosi chake cha kulinda amani nchini Somalia kama hatua ya kujaribu kumbinya rais Pierre Nkurunzinza kuingia katika mazungumzo na wapinzani na kuepusha nchi hiyo kutumbukia katika mgogoro kamili wa kikabila.Hayo yameelezwa hii leo na duru za kidiplomasia.Serikali ya Burundi imepuuza hatua zilizochukuliwa na nchi kadhaa za wafadhili wa Magharibi za kuikatia msaada kama njia ya kutafuta nafasi ya kuishinikiza serikali hiyo kuukomesha mgogoro wa kisiasa wa kiasi mwaka mmoja katika nchi hiyo ya eneo la maziwa makuu barani Afrika. Burundi ina kikosi cha wanajeshi 5400 nchini Somalia chini ya jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika AMISOM.

EgyptAir: Mtekaji ataka kumuona ''mkewe''


Image copyrightAFP
Image captionNdege ya EgyptAir
Ripoti zinasema kuwa mtekaji wa ndege ya EgyptAir anataka kuongea na mkewe walietengana naye anayeishi Cyprus ambaye kwa sasa anadaiwa kuelekea katika uwanja huo wa ndege.
Rais wa Cyprus Nicos Anastasiades amewaambia waandishi wa habari kwamba tukio hilo la utekaji nyara halikuwa la kigaidi,''tunafanya juhudi kuhakikisha kuwa kila mtu anawachiliwa akiwa salama'',aliongezea.
Akijibu maswali ya waandishi iwapo mtekaji huyo alishinikizwa na mapenzi,alicheka na kusema,''kila mara kuna mwanamke anayehusishwa''.
Shirika la habari la Cyprus CYBC linasema kuwa mtekaji huyo huenda alikuwa na malengo yake ya kibinafsi ,mtekaji huyo alikuwa na mkewe waliyetengana nchini Cyprus ,lilisema CYBC.
Walioshuhudia wanasema kuwa mtekaji huyo alirusha barua katika uwanja huo wa ndege ilioandikwa kiarabu akiomba ipelekwe kwa mwanamke huyo.
Image copyrightepa
Image captionNdege ya EgyptAir
Mtaalam wa maswala ya angani David Learmont ameiambia BBC kwmba rubani huyo angekataa kufuata amri ya mtekaji huyo.
''Tunaona kitu kisicho cha kawaida hapa.Rubani aliyetii amri ya mtekaji huyo kwa kuambiwa kwamba kulikuwa na mtu aliyvaa vilipuzi angekuwa na ushahidi wa kutosha kujua kwamba haingewezekana na kwamba hasingefuata amri ya mtekaji huyo."
Image result for FBI

Vita vya aina yake vya kisheria vilivyokuwa vimeanzishwa na serikali ya rais Obama dhidi ya kampuni kubwa la teknologia ya kisasa la Apple vimemalizika ghafla baada ya shirika la upelelezi wa ndani nchini Marekani FBI kusema kwamba limetumia mbinu zake bila ya msaada wa kampuni hiyo kuzidaka taarifa zote zilizokuwa ndani ya simu aina ya Iphone ya mshambuliaji aliyewafyetulia watu risasi katika jimbo la Carlifonia.Hata hivyo hatua hiyo ya FBI  haijafahamika ikiwa inaweza kuathiri mustakabali wa suala la kulindwa kwa mambo binafsi ya mtu.Waendesha mashataka wa serikali hapo jana walimtolea mwito jaji wa serikali kuu  kuifuta amri iliyoibua mvutano ya kuilazimisha kampuni ya Apple kutoa ushirikiano kwa FBI kuvunja simu ya Iphone ya mshambuliaji huyo Syed Farook aliyefariki pamoja na mkewe baada ya kupigwa risasi katika mapambano ya ufyetulianaji risasi na polisi baada ya watu hao wawili kuua watu 14 katika mji wa San Bernardino mwezi Desemba mwaka jana.