Sunday, March 20, 2016

LIST YA WACHEZAJI WATANO WA AFRIKA WANAONGOZA REKODI YA UFUNGAJI KWA MUDA WOTE EPL.
Mchezaji kutoka Afrika ili aweze kucheza Ligi Kuu Uingereza moja kwa moja mara nyingi hadi taifa lake liwe katika viwango vya juu vya FIFA, vinginevyo lazima apite Ligi nyingine barani Ulaya ndio apate nafasi ya kucheza Uingereza.
March 19 mtu wangu wa nguvu kutoka sokka.com nimekutana na list ya rekodi ya wachezaji watano wa kiafrika waliopata bahati ya kucheza Ligi Kuu Uingereza na kuweka rekodi ya kuwa katika TOP 5 ya wachezaji wa Afrika wanaoongoza kwa ufungaji kwa muda wote EPL.
5- Nwankwo Kanu– magoli 54 (Nigeria)Kanu amewahi kuvichezea vilabu vya Arsenal,West Brom and PortsmouthKanu pia amewahi kushinda mataji ya mchezaji bora wa Afrika mara mbili, Ligi ya Mabingwa Ulaya  mara moja na mataji matatu ya FA.
nwankwo-kanu-nigeria_1ih2a1t7pmh0b1aqx30hf58zo1
Nwankwo Kanu
4-Yaya Toure – magoli 55 (Ivory Coast). Baada ya kuondoka FC Barcelona mwaka 2010 na kujiunga na Man City ya Uingereza, staa huyo nyota yake imezidi kung’aa, kwani  kwa kiungo kuwa na idadi hiyo ya magoli inatajwa kuwa sio mbaya.
Fulham-v-Manchester-City-Yaya-Toure-hat-trick_3105609 (1)
Yaya Toure
3- Yakubu Aiyegbeni– magoli 96 (Nigeria). Nyota yake iling’aa msimu wa 2002/2003 katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na klabu ya Maccabi Haifa ndio alipopata nafasi ya kuanza kucheza Uingereza kwa mkopo akiwa na klabu ya Portsmouth na baadae vilabu vya  MiddlesbroughEverton na Blackburn Rovers.
Striker_Yakubu_urges_Blackburn_Rovers_fans_to_stick_together_120341_290454759
Yakubu Aiyegbeni
2- Emmanuel Adebayor – magoli 97 (Togo)Sheyi Emmanuel Adebayor ambaye alizaliwa  26 February 1984 Lome,Togo kutoka kwa wazazi wenye asili ya Nigeria, amempiku Yakubu baada ya kufunga goli lake la kwanza akiwa na Crystal Palace hivi karibuni. Adebayor amewahi kucheza vilabu vya Uingereza kama   ArsenalManchester City na Tottenham.
emmanuel-adebayor
Emmanuel Adebayor
1- Didier Drogba– magoli 104 (Ivory Coast)Drogba amefanikiwa kufunga magoli 104 na kuwa mwafrika anayeoongoza kwa magoli mengi Ligi Kuu Uingereza akiwa ameichezea klabu moja tu Uingereza ChelseaAdebayor bado anayo nafasi ya kumpiku Drogba kwani bado anacheza Uingereza.
Didier Drogba - Cote d Ivoire /CoreeduSud - Match Amical - Foot Football - 03.03.2010 - hauteur attitude
Didier Drogba

No comments:

Post a Comment