Moja kwa Moja: Uchaguzi wa marudio Zanzibar.
08:50 Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar Dkt Ali Mohammed amezungumza na wanahabari baada ya kupiga kura yake katika kituo cha Bungi, Kibera kisiwani Unguja.
Mwanzo amezungumzia hatua ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia uchaguzi huo.
Kuhusu amani na utulivu, amesema anaamini kutakuwa na utulivu visiwani.
08:13 Kumbuka, Chama cha Wananchi (CUF) kilitangaza kwamba hakitashiriki uchaguzi wa marudio unaoendelea leo. Chama hicho kinaamini kilishinda uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana na mgombea wake Maalim Seif Hamad anafaa kutangazwa mshindi.
Tume ya uchaguzi Zanzibar hata hivyo ilitangazwa kwamba hakuna aliyejiondoa rasmi kutoka kwa uchaguzi wa leo.
08:00 Maafisa wa usalama wakishika doria mjini Chake kisiwani Pemba.
07:50 Safari zote za meli kati ya bandari ya Dar es Salaam na visiwa vya Zanzibar zimekatizwa.
Hapa chini ni tangazo la kuwapasha wateja wa Azam Sealink kwamba hakutakuwa na safari za meli kuanzia tarehe 18 hadi 22 Machi kutokana na uchaguzi unaoendelea Zanzibar.
Licha ya kukatizwa kwa safari, badi wapo watu waliojitokeza wakitarajia kusafiri. Wengi wa waliofika ni wageni kutoka Ulaya ambao hawakuwa na habari.
No comments:
Post a Comment