Thursday, March 3, 2016

Mwandishi ''wa al-Shabab'' ahukumiwa kifo.


Image copyrightn
Image captionWapiganaji wa al-shabab
Mahakama ya kijeshi katika mji mkuu wa Somalia,Mogadishu imempatia hukumu ya kifo mwandishi anayedaiwa kupanga njama ya mauaji ya waandishi wengine nchini humo.
Hassan Hanafi,ambaye ni mwanachama wa kundi la kigaidi la al-Shabab alikamatwa nchini Kenya mnamo mwezi Agosti akitoroka.
Mahakama iliamuru kwamba anafaa kuuawa kwa kupigwa risasi.
Upande wa Mashtaka ulimshtumu kwa kuwaua waandishi wengine maarufu nchini Somalia mwaka 2007.
Hanafi alijiunga na wapiganaji wa kundi la al-Shabab miaka michache iliopita baada ya kufanya kazi na Redio Andalus,ambayo ndio inayotoa taarifa za kundi hilo.
Kukingana na kamati inayowalinda waandishi katika shirika la waandishi duniani,waandishi 59 wameuawa nchini Somalia tangu mwaka 1992 na 33 tangu mwaka 2007.

No comments:

Post a Comment