Thursday, March 10, 2016


Image result for Luiz Inacio Lula da Silva
Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, amefunguliwa rasmi mashtaka ya usafirishaji fedha kwa njia haramu, katika uchunguzi unaoendeshwa na waendesha mashitaka wa jimbo la Sao Paulo. Serikali ya jimbo hilo inasema inaituhumu familia ya Lula kumiliki nyumba moja ambayo haijaitangaza kwenye mji wa pwani wa Guaruja. Ijumaa iliyopita, wachunguzi kutoka serikali kuu ya shirikisho walimkamata kwa muda mfupi rais huyo wa zamani kwa mahojiano kwenye kituo cha polisi kwa tuhuma kama hizo. Lula amekanusha kufanya kosa lolote na kwamba anamiliki nyumba hiyo iliyojengwa na kampuni ya ujenzi ya OAS, moja ya makampuni yanayotajwa kwenye kashfa kubwa kabisa ya ufisadi katika shirika la mafuta la Brazil, Petrobras. Mawakili wake wanasema shutuma hizo ni jitihada za mwendesha  mashitaka mkuu Cassio Conserino kuchafua jina la Rais Lula.

No comments:

Post a Comment