Kamanda wa IS auwawa karibu na Raqa,Syria
Shambulizi lililofanywa na ndege isiyokuwa na rubani karibu na eneo linalodhibitiwa na kundi la kigaidi la dola la kiislamu Raqa limesababisha kifo cha kamanda wa kundi hilo la jihadi aliyekuwa akielekea mkoa wa Aleppo kutokana na maelezo ya mkuu wa kundi hilo.Taarifa hizo zimetolewa leo na kundi linalofuatilia hali ya Syria.Kifo cha kamanda huyo ni tukio la karibuni kabisa kati ya msururu wa matukio ya kushambuliwa kwa kundi hilo la jihadi katika kipindi cha wiki za hivi karibuni na limekuja siku kadhaa baada ya vikosi vya serikali vinavyosaidiwa na Urusi kuudhibiti tena mji wa kale wa Palmyra.Kamanda huyo wa ngazi ya juu wa IS Abu al-Hija raia wa Tunisia aliuwawa jana usiku katika shambulio la ndege isiyokuwa na rubani iliyoongozwa na kikosi kinachosimamiwa na Marekani,limesema shirika linalofuatilia haki za binadamu nchini Syria lenye makao yake London.Aidha shirika hilo limesema kamanda huyo alisafiri kwenda Syria kutoka Iraq kwa maagizo ya kiongozi wa IS Abu Bakr al Baghadadi, katika kipindi cha masaa 24 kabla ya kifo chake.
No comments:
Post a Comment