Korea Kaskazini yajibu vikwazo vya UN.
Korea Kaskazini imerusha makombora ya masafa mafupi, baharini kujibu vikwazo vipya ilivyowekewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Jeshi la Korea Kusini limethibitisha kushuhudia shughuli hiyo na kusema haikulenga yeyote. Wadadisi wameonya kutokea taharuki kwenye rasi ya Korea kutokana na vikwazo hivyo.
Korea Kaskzini ilifanya majaribio ya nyuklia hapo mwakani. Chini ya vikwazo vipya mizigo yote inayoingia Korea Kaskazini kutoka nje itaanza kukaguliwa, huku watu kadhaa na mashirika yakiwekewa vikwazo.
No comments:
Post a Comment