Njia ya juu yaporomoka India, 10 wauawa, zaidi ya 150 wakwama
Watu wasiopungua 10 wameuawa katika mji wa mashariki mwa India wa Kolkata leo na wengine 150 wanahofiwa kukwama baada ya kuporomoka kwa njia ya juu iliyokuwa inajengwa na kuangukia magari yanayotembea kwenye barabara ya chini. Polisi imesema asakri wa zimamoto pamoja na wakaazo walikuwa wanajaribu kuwaokoa watu waliofunikwa na vifusi vya njia hiyo iliyoporomoka. Afisa wa polisi Raichand Mohta, amesema hali ni mbaya na kwa wakati hakuna anaejuwa ni watu wangapi wamekwama. Njia hiyo hiyo ya juu imekuwa ikijengwa tangu mwaka 2009 na imekuwa ikikosa muda wake wa kukamilishwa kwa mara kadhaa. Miradi ya ujenzi nchini India huwa inakumbwa na ukosefu wa viwango vya usalama.
No comments:
Post a Comment