Thursday, March 31, 2016

Chama chatisha kumuondoa Zuma madarakani


Image copyright
Image captionRais Jacob Zuma
Chama cha Democtratic Alliance nchini Afrika Kusini kumeanzisha kampeni ya kumuondoa rais Jacob Zuma madarakani baada ya mahakama ya kikatiba kutoa uamuzi kuwa alikiuka katiba.
Mahakama ilipata kuwa bwana Zuma alikataa kutii agizo kutoka kwa ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu mwaka 2014 la kamtaka alipe pesa zilizotumika kuifanyia ukarabati nyumba yake ya kibinafsi.
Image copyrightGetty
Image captionNyumba ya Zuma ya Nkandla
Vyama viwili vya upinzani viliwasilisha kesi hiyo mahakamani ili kumlazimu rais Jacob Zuma kuzingatia matokeo ya uchunguzi yaliofanywa na mkaguzi wa hesabu za serikali, kwamba alihusika na mabadiliko yaliofanyiwa nyumba yake ya Nkandla.
Mamilioni ya madola yalitumika katika kile kilitajwa na serikali kuwa uimarishaji wa usalama. Marekebisho hayo yalishirikisha ukumbi,kidimbwi cha kuogelea na zizi la ngombe

No comments:

Post a Comment