Thursday, March 3, 2016

Wahamiaji haramu wakatazwa kuingia Ulaya.



Image copyrightReuters
Image captionWaziri mkuu wa Ugiriki Alexi Tsipras na rais wa baraza la Ulaya Donald Tusk

Rais wa baraza la Ulaya Donald Tusk amewaonya wahamiaji haramu wa kiuchumi dhidi ya kuelekea Ulaya, katika harakati mpya za kutatua mgogoro wa wahamiaji Ulaya.
Amesema kuwa wahamiaji haramu wa kiuchumi wanahatarisha maisha na fedha zao.
Bwana Tusk yuko ziarani Ugiriki na Uturuki ili kujaribu kupata makubaliano ya kupunguza ongezeko la wahamiaji wanaoelekea magharibi.
Zaidi ya wahamiaji 25,000 wamewachwa bila makao nchini Ugiriki kupitia kuimarisha udhibiti wa mipaka na kuongeza hofu ya mgogoro wa kibinaadamu.

Image copyrightGetty
Image captionWahamiaji

Siku ya Alhamisi ,kundi la wahamiaji liliziba barabara moja ya reli katika upande wa mpaka wa Ugiriki unaopakana na Macedonia ili kupinga vikwazo hivyo.
Masharti hayo yaliafikiwa baada ya Austria na mataifa mengine ya kuvunjika kwa Urusi kuamua kuwaruhusu wahamiaji wa Syria na Iraqi kupitia nchi zao.
Hatua hiyo iliwazuia maelefu ya raia wanaotaka kuingia Ulaya bila vibali,ikiwemo raia wa Afghanistan pamoja na wale wanaodaiwa kuwa wahamiaji wa kiuchumi.

No comments:

Post a Comment