Ethiopia yawaomba radhi jamii ya Oromo.
Waziri mkuu wa Ethiopian, Hailemariam Desalegn,ameomba msamaha kwa tukio ambapo vikosi vya usalama vilikabiliana na raia jamii ya wa - Oromo na kuuawa kwa watu zaidi ya 250.
Hata hivyo amelaumu watu aliowaita wasiopenda amani kwa maafa hayo yaliyotokea.
Katika taarifa ya moja kwa moja kupitia televisheni amedai kuwa watu wa itikadi kali wamejaribu kupanda mbegu za chuki baina ya jamii tofauti ambazo zimeishi kwa amani kwa miaka mingi
nchini humo na kuongeza kuwa serikali yake itawachukulia hatua kali.
Maandamano yamekuwa yakiendelea dhidi ya hatua ya utawala kutaka kufanya upanuzi wa mji wa mkuu Addis Ababa ambao ungemegua baadhi ya maeneo ya wanavijiji wa Oromo, japo hatua hiyo ilisitishwa tangu mwezi January.
Wachambuzi wanasema japo Oromo ndio jamii kubwa zaidi nchini Ethiopia, wanalalamikia kile wanachokiita ukandamizwaji ukiwemo wa lugha yao ya Amharic.
No comments:
Post a Comment