Tuesday, March 29, 2016

Image result for FBI

Vita vya aina yake vya kisheria vilivyokuwa vimeanzishwa na serikali ya rais Obama dhidi ya kampuni kubwa la teknologia ya kisasa la Apple vimemalizika ghafla baada ya shirika la upelelezi wa ndani nchini Marekani FBI kusema kwamba limetumia mbinu zake bila ya msaada wa kampuni hiyo kuzidaka taarifa zote zilizokuwa ndani ya simu aina ya Iphone ya mshambuliaji aliyewafyetulia watu risasi katika jimbo la Carlifonia.Hata hivyo hatua hiyo ya FBI  haijafahamika ikiwa inaweza kuathiri mustakabali wa suala la kulindwa kwa mambo binafsi ya mtu.Waendesha mashataka wa serikali hapo jana walimtolea mwito jaji wa serikali kuu  kuifuta amri iliyoibua mvutano ya kuilazimisha kampuni ya Apple kutoa ushirikiano kwa FBI kuvunja simu ya Iphone ya mshambuliaji huyo Syed Farook aliyefariki pamoja na mkewe baada ya kupigwa risasi katika mapambano ya ufyetulianaji risasi na polisi baada ya watu hao wawili kuua watu 14 katika mji wa San Bernardino mwezi Desemba mwaka jana.

No comments:

Post a Comment