Tuesday, March 29, 2016


Image result for UMOJA WA ULAYA
Umoja wa Ulaya unapanga kuiondolea Burundi msaada wa fedha za kusimamia kikosi chake cha kulinda amani nchini Somalia kama hatua ya kujaribu kumbinya rais Pierre Nkurunzinza kuingia katika mazungumzo na wapinzani na kuepusha nchi hiyo kutumbukia katika mgogoro kamili wa kikabila.Hayo yameelezwa hii leo na duru za kidiplomasia.Serikali ya Burundi imepuuza hatua zilizochukuliwa na nchi kadhaa za wafadhili wa Magharibi za kuikatia msaada kama njia ya kutafuta nafasi ya kuishinikiza serikali hiyo kuukomesha mgogoro wa kisiasa wa kiasi mwaka mmoja katika nchi hiyo ya eneo la maziwa makuu barani Afrika. Burundi ina kikosi cha wanajeshi 5400 nchini Somalia chini ya jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika AMISOM.

No comments:

Post a Comment