Sunday, March 20, 2016

NEC WAYAZUNGUMZA HAYA BAADA YA KUJITOA KWA MGOMBEA UBUNGE WA CUF JIMBO LA KIJITOUPELE ZANZIBAR.
chaguzi Mkuu wa october 2015 ulikuwa ni uchaguzi uliovuta hisia za wengi na idadi kubwa ya watu walihamasika kushiriki uchaguzi huo. Licha ya Uchaguzi kufanyika kwa mafanikio makubwa katika maeneo mengi kulikuwa na majimbo ambayo uchaguzi wa wabunge uliahirishwa kutokana na sababu mbalimbali likiwemo jimbo la KijitoupeleZanzibar.
Uchaguzi wa Jimbo la Kijitoupele umepangwa kufanyika kesho sambamba na uchaguzi wa marudio Zanzibar. Leo March 19 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian Lubuva amekutana na wanahabari na kujibu swali kuhusiana na kujitoa kwa mgombea kwenye Uchaguzi huo, Lubuva amesema……..
>>>’kama mtu anafanya tu kienyeji kwa kutoa taarifa kwamba hatoshiriki na ni muda ambao haulingani na matakwa ya kikatiba na sheria, kwa hiyo mchakato unaendelea na katika hali hiyo, huyo mgombea na wengine watakuwa bado wapo kwenye fomu zetu’:-Damian Lubuva
Aidha Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ‘NEC’ Kailima Ramadhaniamefafanua kuhusu kujitoaa kwa CUF kwenye uchaguzi wa jimbo la KijitoupeleZanzibar….
>>>’ni kweli tumepokea barua ya CUF kujitoa kwenye uchaguzi wa kijitoupele lakini kwa mujibu wa sheria hawakufuata taratibu za kujitoa  kwa hiyo Tume ya Uchaguzi inamtambua kwamba ni mgombea halali na kura zake atapewa baada ya uchaguzi‘:-Kailima Ramadhani
Lubuva pia amewatoa wasiwasi wananchi kuwa ulinzi na usalama wa wapiga kura upo wa kutosha hivyo amewaomba wananchi wajitokeze kupiga kura

No comments:

Post a Comment