Mazungumzo ya amani kati ya upande wa serikali na waasi nchini Syria yanatarajiwa kuanza Machi 7, mwaka huu iwapo hatua ya kusimamisha mapigano ambayo utekelezaji wake ulitarajiwa kuanza rasmi usiku huu itadumu kwa muda uliopangwa. Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika mgogoro huo wa Syria, Steffan de Mistrura alitangaza tarehe hiyo mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa muda mchache kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa makubaliano ya kusimamisha mapigano nchini Syria yaliyofikiwa na Marekani pamoja na Urusi na kuridhiwa pia na upande wa serikali nchini Syria pamoja na makundi ya waasi. de Mistura aliongeza kuwa kuanza tena kwa mazungumzo hayo ya amani ya Syria kutategemea pia misaada ya kiutu kuendelea kuwafikia raia nchini humo katika kipindi hicho. Hata hivyo hatua hiyo ya kusimamisha mapigano haizuii mashambulizi kuendelea dhidi ya kundi la dola la kiisilamu pamoja na makundi mengine ya itikadi kali likiwemo kundi la Al-Nusra Front ambalo linamahusiano na kundi la Al-qaeda.
No comments:
Post a Comment