Iran, Ujerumani zataka ushirikiano kupambana na ugaidi.
Iran na Ujerumani zimekubaliana kuhusu haja ya kuwa na ushirikiano kupambana na ugaidi. Hayo yamebainika leo wakati waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier akiwa afisa wa ngazi ya juu wa hivi karibuni kufanya ziara nchini Iran tangu kuanza kutekelezwa kwa makubaliano ya kihistoria ya nyuklia.
Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema nchi hizo mbili zinaweza kushirikiana katika kutatua mizozo ya kikanda na kimataifa, hususan katika kupambana na ugaidi. Rouhani amesema hali ya upatikanaji wa silaha na fedha kwa ajili ya ugaidi ni lazima ikomeshwe.
Ziara ya Steimeier imekuja baada ya makubaliano ya kihistoria kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani kuweka ukomo katika mpango wa kinyuklia wa Iran ili kuweza kuondolewa vikwazo vya kimataifa.
Waziri Steinmeier atakwenda Saudi Arabia baada ya ziara hiyo nchini Iran.
No comments:
Post a Comment