Wednesday, February 17, 2016


Image for the news result

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa aliyekuwa Katibu mkuu Boutros Boutros-Ghali amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 93. Mmisri huyo, aliyekuwa katibu mkuu wa kwanza kutoka Afrika pamoja na Ulimwengu wa Kiarabu, alifariki dunia jana mjini Cairo, kutokana na maradhi yasiyojulikana. Boutros-Ghali ambaye alizaliwa katika mji mkuu wa Misri mnamo mwaka wa 1922, aliliongoza shirika hilo la kimataifa kuanzia mwaka wa 1992 hadi 1996. Wakati akisifiwa kwa operesheni ya kwanza kubwa ya msaada wa dharura kuwahi kufanywa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuwaisaidia waathiriwa wa baa la njaa nchini Somalia, uongozi wake ulikosolewa kutokana na Umoja wa Mataifa kushindwa kuchukua hatua wakati wa mauaji ya halaiki nchini Rwanda mwaka wa 1994 na kushindwa kwake katika kutafuta uungwaji mkono kwa Umoja wa Mataifa kuingilia kati katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Angola vya miaka ya 1990.

No comments:

Post a Comment