Saturday, February 20, 2016


Image result for wanamgambo wa TAK
Kundi dogo la wanamgambo wa Kikurdi nchini Uturuki limedai kuhusika katika shambulizi la bomu lililofanyika wiki hii mjini Ankara, ambalo lililenga msafara wa magari ya kijeshi na kuwaua watu 28. Kundi la Kurdistan Freedom Falcons, TAK, lililojitenga kutoka kundi la PKK limesema lilifanya shambulizi hilo kulipiza kisasi dhidi ya mashambulizi ya jeshi la serikali kusini mashariki mwa nchi hiyo, ambayo yamesababisha uharibifu mkubwa. Mapigano kati ya wanajeshi wa Uturuki na wanamgambo wa Kikurdi yamesababisha watu kadhaa kuuawa na maelfu kuyahama makaazi yao katika mji wa Cizre. Madai hayo ya TAK yanakinzana na madai ya serikali ya Uturuki kuwa wanamgambo wa Kikurdi wa Syria wanaoungwa mkono na Marekani ndio walihusika katika shambulizi hilo la Ankara. Kundi hilo la wanamgambo wa Kikurdi limewaonya watalii kutotembelea Uturuki likisema halitawajibika kwa watakaouawa katika mashambulizi yatakayofanyika katika maeneo ya watalii.

No comments:

Post a Comment