Wednesday, February 17, 2016

Chanongo, Ubwa warudi kwa Mfaransa.

Mchezaji wa Stand United, Haruni Chanongo 
Jana Jumatatu, wachezaji hao walikuwa miongoni mwa wachezaji waliokwenda kambini kwa ajili ya mechi yao ijayo ambapo wataikaribisha JKT Ruvu, mechi itakayopigwa Uwanja wa CCM Kambarage, kambi hiyo imewekwa kwenye mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama, Shinyanga.

WACHEZAJI wa Stand United, Haruni Chanongo na Abuu Ubwa, wamejiunga na kikosi hicho ambapo juzi Jumapili walimalizana na kocha wao, Patrick Leiwig na kujiunga na kambi ya Mfaransa huyo.
Jana Jumatatu, wachezaji hao walikuwa miongoni mwa wachezaji waliokwenda kambini kwa ajili ya mechi yao ijayo ambapo wataikaribisha JKT Ruvu, mechi itakayopigwa Uwanja wa CCM Kambarage, kambi hiyo imewekwa kwenye mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama, Shinyanga.
Hivi karibuni wachezaji hao waliondoka kambini bila ruhusa ya Leiwig na kwenda kufanya majaribio klabu ya TP Mazembe na habari za ndani kutoka kwenye klabu hizo zinadai kuwa wachezaji hao hawajafuzu majaribio hayo na hivyo wamelazimika kurudi kujiunga na timu yao ambapo tayari wamekosa mechi tano mpaka sasa.
Kocha Msaidizi wa Stand United, Athumani Bilali, aliliambia Mwanaspoti kuwa kabla ya hapo, Leiwig alikutana na wachezaji hao ambao waliingia Shinyanga Ijumaa iliyopita na kumaliza tofauti zao kwani awali Mfaransa huyo alisema hataki tena kuwaona kwenye kikosi chake.
“Jana (juzi) Jumapili, walikaa na kumalizana ndiyo maana tumekuja nao kambini, nafikiri yameisha ana atawatumia kwenye mechi zijazo akiona wapo fiti,” alisema Bilali.     

No comments:

Post a Comment