Jeshi la Kenya latangaza kumuua kamanda wa Al Shabab.
Jeshi la Kenya limesema limemuua mkuu wa masuala ya kijasusi wa kundi la waasi wa Somalia la Al Shabab na makamanda wengine kumi katika shambulizi la anga nchini Somalia. Taarifa kutoka jeshi la Kenya imesema wanajeshi wa Kenya ambao ni sehemu ya kikosi cha Umoja wa Afrika kinachopambana dhidi ya waasi hao wa Al Shabab nchini Somalia wamemuua kamanda mwandamizi na mkuu wa ujasusi wa kundi hilo Mahad Karate katika shambulizi kubwa.
No comments:
Post a Comment