Wednesday, February 3, 2016


Image result for obama
Miaka  saba  ndani  ya  utawala  wake , rais Barack Obama atafanya  ziara  yake  ya  kwanza  katika  msikiti  nchini Marekani  leo, akitoa ishara  ya  kupinga  matamshi  makali ya  wagombea  wa  chama  cha  Republican  dhidi  ya Waisilamu.
Obama  ambaye  babu  yake  alibadili  dini  na  kuwa Muislamu , atafanya  ziara  hiyo  fupi  katika  msikiti  mjini Baltimore , ambako  atakutana  na  viongozi  wa  jamii  ya Waislamu na  kutoa  hotuba  fupi.
Aliwahi  kutembelea  misikiti  nchini  Malaysia  , Indonesia na  Misri  akiwa  rais, lakini  bado  hajawahi  kutembelea msikiti  nchini  Marekani.
Sera  za  mambo  ya  kigeni  za  Obama  zimelenga  katika kuimarisha  mahusiano  na  mataifa  ya  Kiislamu, kuanzia kufikia  makubaliano  na  Iran na  kuwa  na  mahusiano mazuri  na  Indonesia   na  kumaliza  vita  nchini  Iraq  na Afghaninistan.

No comments:

Post a Comment