George Bush amfanyia kampeni nduguye.
Aliyekuwa rais George W Bush ameanza kampeni za kumpiga jeki nduguye mdogo Jeb ambaye hafanyi vizuri katika uteuzi wa mgombea wa urais kupitia chama cha Republican.
Alikutana na wakongwe na kuhudhuria mkutano katika jimbo la Carolina Kusini siku ya jumatatu,kabla ya uchaguzi wa jimbo hilo unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi.
Uongozi wa George Bush umeshtumiwa na mgombea wa Republican aliye kifua mbele Donald Trump.
Jeb Bush ,aliyekuwa Gavana wa Florida ametumia fedha nyingi za kampeni lakini hajafaulu katika kampeni.
Anajaribu kumfikia Trump na Seneta Ted Cruz,ambaye alishinda katika jimbo la New Hampshire na Iowa.
Familia ya bwana Bush haijajihusisha moja kwa moja na kempaeni ya Jeb ,na mwaka uliopitiza alisisitiza kwamba anagombea binafsi wadhfa huo.
Lakini wiki iliopita mamaake Barbara Bush,mkewe aliyekuwa rais George HW Bush,alimuunga mkono.
No comments:
Post a Comment