Sunday, February 21, 2016


Waziri mkuu mteule wa Libya Fayez al Sarraj amewasilisha hapo jana mpango wa serikali yake mpya ya umoja wa kitaifa kwa bunge linalotambulika na Jumuiya ya kimataifa kabla ya kupigiwa kura na wabunge kuiidhinisha. Shirika la habari la Libya LANA limeripoti kuwa wabunge wamejadili na baraza la Rais kuhusu mpango huo uliopendekezwa wa serikali hiyo mpya na orodha ya majina ya mawaziri. Kikao hicho cha bunge kiliahirishwa baada ya mjadala mkali na bunge linatarajiwa kukutana tena leo. Umoja wa Mataifa umekuwa ukiyashinikiza mabunge mawili yanayopingana Libya kuunga mkono kuundwa kwa serikali ya muungano. Libya imekumbwa na msukosuko na kutokuwa na serikali thabiti tangu mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment