Sunday, February 21, 2016


Wapiga kura nchini Niger leo wanashiriki katika uchaguzi mkuu ambao wafuasi wa Rais Mahamadou Issoufuo wana imani atashinda muhula wa pili wa miaka mitano kwa misingi ya kuwa na rekodi nzuri ya kuimarisha usalama nchini humo. Uchaguzi huo wa leo unakuja wakati ambapo mahakama ya juu ya Niger imeidhinisha mpango tete wa kuwaruhusu wapiga kura wasio na vitambulisho, ilimradi waambatane vituoni na watu wawili wanaowafahamu. Muungano wa vyama vya upinzani umepinga hatua hiyo na kuitaja njama ya serikali kuhujumu uchaguzi. Mgombea urais wa upinzani Amadou Boubacar Cisse amesema uamuzi huo wa mahakama ni matumizi mabaya ya mamlaka na ukiukaji wa sheria za uchaguzi. Rais Issoufuo anakabiliwa na ushindani kutoka kwa wagombea wengine 14.

No comments:

Post a Comment