Tuesday, February 16, 2016


Maandamano makubwa ya wanafunzi nchini India kuwahi kushuhudiwa katika robo karne yalisambaa jana katika vyuo vikuu kote nchini humo baada ya kukamatwa kiongozi wa wanafunzi kwa tuhuma za fitina, ikiwa ni mapambano ya karibuni dhidi ya serikali ya Waziri Mkuu Narendra Modi kuhusu uhuru wa kujieleza. Kukamatwa kwa Kanhaiya Kumar anayeegemea siasa za mrengo wa kushoto, ambaye alikuwa ameandaa mkutano wa kumbukumbu ya kuuliwa kwa kiongozi mmoja aliyepigania kujitenga jimbo la Kashmir mnamo mwaka wa 2013, kumesababisha maandamano katika karibu vyuo vikuu 18. Maelfu ya wanafunzi walisusia masomo na kuweka vizuizi barabarani kwa siku ya nne mfululizo. Waziri Mkuu Modi ameitetea hatua ya kukamatwa kwa kiongozi huyo wa wanafunzi, wakati wachambuzi wa masuala ya kisiasa wakiishutumu serikali kwa kuukandamiza uhuru wa kujieleza.

No comments:

Post a Comment