Tuesday, February 16, 2016

Majengo ya shirika la utangazaji Kenya yatwaliwa.


Image result for SHIRIKA LA UTANGAZAJI KENYA

erikali ya Baraza la Jiji la Nairobi imetwaa majengo ya shirika la utangazaji la Kenya (KBC) kutokana na kutolipiwa kodi.
Baraza hilo limeweka bango kubwa katika lango la majengo hayo kutangaza kwamba kwa sasa majengo hayo yamo chini ya usimamizi wa baraza hilo.
"Wapangaji wote wanafaa kulipa kodi kwa Baraza la Jiji hadi malimbikizi ya kodi yalipwe,” tangazo la baraza hilo linasema.
Baraza la jiji linasema linadai kodi ya jumla ya $20 milioni (Shilingi bilioni mbili za Kenya).
Hii si mara ya kwanza kwa baraza hilo kutwaa usimamizi wa majengo jijini Nairobi kutokana na kutolipiwa kodi lakini huwa nadra sana kwa mashirika ya serikali kuandamwa.
Shirika hilo la utangazaji limekuwa likikabiliwa na matatizo ya kifedha miaka ya karibuni.

No comments:

Post a Comment