Sunday, February 21, 2016


Waziri mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin Archange Touadera ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais hapo jana, katika uchaguzi unaotarajiwa kuwa muhimu katika kukomesha ghasia nchini humo. Touadera alishinda duru ya pili ya uchaguzi wa rais dhidi ya mpinzani wake Anicet George Dologuele kwa asilimia 62.71 ya kura. Mahakama ya kikatiba inatarajiwa kuthibitisha matokeo hayo.

No comments:

Post a Comment