Monday, February 22, 2016

Nywele ya John Lennon yauzwa kwa dola 35,000!


Image copyrightAP
Image captionShungi la nywele ya msanii nguli wa kundi la ''The Beatles'' John Lennon
Shungi la nywele ya msanii nguli wa muziki chapa Rock na muanzilishi wa kundi la ''The Beatles'' John Lennon aliyeaga dunia miaka 36 iliyopita imeuzwa kwa dola elfu thelathini na tano ($ 35,000) katika mnada mmoja huko Marekani.
Kinyozi wa Muimbaji huyo maarufu kote duniani alificha shungi la nywele baada ya kumnyoa msanii huyo alipokuwa akijiandaa kuigiza katika filamu moja.
Lennon aliuuawa mwaka wa 1980 mjini New York Marekani.
Mnunuzi mmoja shabiki sugu wa Lennon kutoka Uingereza ndiye aliyeandika hundi hiyo ya dola ($ 35,000).
Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionLennon aliuuawa mwaka wa 1980 mjini New York Marekani.
Bidhaa zingine zilizotumika na kundi hilo la muziki la ''The Beatles''pia ziliuzwa katika mnada huo huko Texas.
Baadhi ya bidhaa hiyo ilikuwa nakala maalum ya albamu yao ya 'Yesterday and Today', iliyouzwa kwa dola laki moja u nusu ($150,00

No comments:

Post a Comment