Wednesday, February 17, 2016

Petro Poroshenko amtimua waziri mkuu


Image copyrightAFP
Image captionaliyekuwa waziri mkuu wa Ukraine, Arseniy Yatsenyuk
Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko,, amemtaka waziri mkuu wa nchi hiyo kuachilia madaraka, kwa maelezo kwamba amepoteza imani na uungwaji mkono na umma wa nchi hiyo ikiwemo serikali ya muungano.
Kauli ya rais Poroshenko ilikuja muda mfupi kabla waziri mkuu, Arseniy Yatsenyuk, hajalihitubia bunge la nchi hiyo mjini Kiev.
Bwana Yatsenyuk aliwaambia wabunge kwamba baraza lake la mawaziri limejitahidi kutimiza wajibu wake katika wakati mgumu , na kusema kwamba alikuwa akitarajia kupata upinzani mkali na kura ya hapana katika utendaji wake.
Waziri mkuu huyo ameingia lawamani kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya kukithiri kwa rushwa nchini humo.Na katika siku za hivi karibuni lilipitishwa azimio la kumtaka waziri huyo aachilie madaraka kwa kutowajibika ,na hatua hiyo iliibua maswali yasiyokuwa na majibu katika serikali za ukanda wa umoja wa ulaya na hata shirika la fedha ulimwenguni IFM.
Hata hivyo waziri huyo anayekabiliwa na upinzani mkali kutoka katika serikali yake , Arseniy Yatsenyuk, amevuka kikwazo cha kutokuwa na imani naye kutoka kwa wabunge nchini Ukraine, saa kadhaa baada ya rais kumtaka ajiuzulu.
Wabunge mia moja tisini na wanne walimpigia kura ya ndiyo ili asalie madarakani miongoni mwa wabunge miambili na ishirini na sita .

No comments:

Post a Comment