Sunday, February 21, 2016

WAYNE ROONEY AKATAA KUSAJILIWA NA SHANGHAI SHENHUA YA CHINA.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza na nahodha wa klabu ya Man United Wayne Rooney wiki hii aliingia kwenye headlines baada ya klabu ya wachina ya Shanghai Shenhua kuomba kumsajili kutoka klabu yake ya Man United na kwenda kuanza maisha mapya ya soka nje ya Uingereza kwa mara ya kwanza.
Klabu ya Shanghai Shenhua ambayo ilianza kuiomba Man United kumsajili Wayne Rooney kwa dau la pound milioni 27 mwishoni mwa mwaka 2015, kwa sasa inamuhitaji na ilitaka kuwa inamlipa mshahara wa pound 500,000 kwa wiki,  katika mkataba wa miaka mitatu, mshahara ambao ni mara mbili ya anaolipwa na Man United kitu ambacho kingemfanya Wayne Rooney avune zaidi ya Tsh bilioni 220 kwa kipindi cha miaka mitatu nje ya posho na bonansi za mechi.
February 20 Wayne Rooney anaripotiwa na Sunday Times kukataa mpango huo wa kujiunga na klabu hiyo ya China. Kama utakuwa unakumbuka vizuri, klabu ya Shanghai Shenhua iliwahi kuwasajili wachezaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba na Nicolas Anelka, Hivyo Rooney kukataa mpango huo wa kujiunga na klabu hiyo unafananishwa sawa Rooney na kukataa zaidi ya Tsh bilioni 220.

No comments:

Post a Comment