Wednesday, February 24, 2016

Uchumi wa Afrika Kusini uko 'taabani'


Image copyrightReuters
Image captionWaziri wa Fedha Pravin Gordhan
Uchumi wa taifa la Afrika Kusini uko katika hali mbaya,waziri wa fedha nchini humo Pravin Gordhan amesema.
Tamko hilo lilijiri kabla ya hotuba yake ya matumizi ya serikali ambapo alipunguza takwimu za ukuwaji wa uchumi wa taifa hilo kutoka asilimia 1.7 hadi 0.9.
Alikiri kwamba uchumi unazorota kutokana na kupungua kwa ukuaji wake, asilimia 25 ya ukosefu wa ajira na kuenea kwa umasikini.
Sarufi ya Afrika kusini Rand ambayo imeshuka katika kipindi cha miaka mitano ilianguka tena wakati alipokuwa akitoa hotuba hiyo.
Image captionSarufi ya Afrika kusini Rand
Bwana Gordhan alitangaza kuongezeka kwa viwango vya kodi ya ushuru, faida ya mtaji, mafuta, vinywaji vyenye sukari, pombe na tumbaku pamoja na ushuru wa mazingira ambao unatarajiwa kuleta randi bilioni 18 sawa na dola bilioni 1.18.
Alikuwa ametarajiwa kutangaza mipango ya kubinafsisha mali ya serikali,lakini alisema kuwa mipango inaendelea ya kuunganisha shirika la ndege la taifa hilo lenye hasara na shirika la ndege linalomilikiwa na serikali la SA Express.

No comments:

Post a Comment