Mkutano wa NATO Brussels.
Mawaziri wa ulinzi wa NATO wanaokutana mjini Brussels wanajadili vipi jumuiya hiyo itakavyoweza kusaidia kuzuwia wimbi la wahamiaji wanaoingia katika bara la Ulaya.
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Ursula von der Leyen amesema nchi yake itashiriki katika ujumbe unaopendekezwa ukitumia meli kutoka mataifa wanachama wa NATO kujaribu kukamata magenge yanayosafirisha watu kutoka Uturuki kwenda Ugiriki.
Waziri wa ulinzi wa Uingereza Michael Fallon anaunga mkono pendekezo lolote ambalo linaruhusu majeshi ya NATO kuchukua hatua za kuvunja mtandao wa magenge yanayosafirisha watu.
Wakati huo huo , katika mpaka kati ya Uturuki na Syria malori yenye mahitaji kwa ajili ya binadmu yamevuka mpaka na kuingia Syria kupeleka misaada kwa mamia kwa maelfu ya wakimbizi wa Syria ambao wamejazana katika eneo hilo la mpaka.

No comments:
Post a Comment