Utafiti kuhusu virusi vya Zika.
Wanasayansi wa ngazi ya juu duniani kote wameahidi kuchangia kwa haraka na huru data zote, utafiti na utaalamu wao kuhusiana na virusi vya Zika katika juhudi za kupambana na ugonjwa huo.
Mambo mengi hayafahamiki juu ya ugonjwa huo unaombukizwa kupitia mbu, ugonjwa amabo umesababisha hali ya wasi wasi kimataifa, hususan katika mataifa ya Amerika ya kusini na eneo linalopatikana kwa wingi ugonjwa huo nchini Brazil.
Shirika la afya ulimwenguni WHO limetoa maelekezo kwa wanawake, hususan wale ambao ni waja wazito , juu ya kujilinda dhidi ya virusi hivyo.
No comments:
Post a Comment