Thursday, February 18, 2016

Upigaji kura wachelewa maeneo mengi Uganda.


kura
Image captionUpigaji kura unafaa kuanza saa moja asubuhi kwa mujibu wa sheria
Wapiga kura nchini Uganda wanaendelea kupiga kura vituoni kuwachagua viongozi, ingawa katika baadhi ya vituo upigaji kura ulichelewa kuanza.
Hili lilitokana na vifaa na karatasi za kupigia kura kutofikishwa vituo kwa wakati katika baadhi ya maeneo.
Mjini Kampala, ambapo makao makuu ya Tume ya Uchaguzi yapo, bado kuna vituo ambavyo kufikia saa nne upigaji kura haukuwa umeanza.
Hata hivyo, tume hiyo kwenye ukurasa wake wa Twitter, imeandika: "Tunabaki kuwa na matumaini na tunawahikishia kwamba nyote mtaweza kupiga kura leo. Tunasikitika kutokana na kuchelewa huku. Asanteni.”
Kuhusu iwapo muda wa kupiga kura utaongezwa, tume hiyo kupitia mitandao ya kijamii imesema kwa mujibu wa sheria, ni sharti vituo vifungwe saa kumi alasiri.
Tume hiyo imeahidi kuhakikisha wapiga kura wote watakaojitokeza kufikia wakati huo wanapiga kura.
Uchaguzi
Image captionMwangalizi mkuu wa Jumuiya ya Madola Olusegun Obasanjo (kushoto) akizungumza na baadhi ya wapiga kura Kampala
Raia katika maeneo mengi nchini humo pia wanalalamikia kutatizika wakiingia mitandao ya kijamii kama vile Twitter, Facebook na WhatsApp, sana kwa kutumia simu. Serikali haijaeleleza ni nini chanzo cha matatizo hayo.
Kuna wagombea saba wa urais wanaojaribu kuhitimisha uongozi wa Rais Yoweri Museveni ambaye ameongoza kwa miaka 30 sasa.
UgandaImage copyrightReuters
Image captionWapiga kura katika kituo cha Kirihura, magharibi mwa Uganda
Wanaotoa ushindani mkubwa kwa Bw Museveni ni mgombea wa FDC Kizza Besigye na waziri mkuu wa zamani Amama Mbabazi.
Kuna jumla ya wapiga kura 15 milioni ambao wamejisajili kupiga kura nchini humo kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi.

No comments:

Post a Comment