Saturday, February 20, 2016

MOJA KWA MOJA: Matokeo ya uchaguzi Uganda.




12:57 Mwangalizi mkuu wa Umoja wa Ulaya Eduard Kukan amesema hakuna ushahidi wa kuonyesha kwamba Tume ya Uchaguzi Uganda ilijifunza kutokana na yaliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu 2011.
15:57 Mwangalizi mkuu wa Bunge la Ulaya Bw Leinen amesema kuna hatua nyingi ambazo zinafaa kuchukuliwa kuboresha uchaguzi Uganda.
12:04 Mwangalizi mkuu wa Bunge la Ulaya Jo Leinen asema kulikuwa na kasoro nyingi. Asema mfano fedha za serikali na chama lazima zitenganishwe. Asema hakukuwa na usawa katika kuwapa wagombea nafasi katika vyombo vya habari vya dola. Asema tume pia haikuwapasha raia habari vyema.
11:57 Waangalizi wa Umoja wa Ulaya: Tutatoa ripoti kamili baadaye ambayo pia itakuwa na mapendekezo ya hatua zinazofaa kuchukuliwa kuboresha mfumo wa uchaguzi Uganda.
11:56 Waangalizi wa Umoja wa Ulaya: Hatua ya kufunga usajili wa wapiga kura Mei 11 uliwafungia watu waliotimiza umri wa miaka 18 baada ya tarehe hiyo.
11:54 Hakuna mfumo wa kisheria wa kuhakikisha usawa wakati wa kampeni. Sheria za kufichua fedha za kampeni hazifuatwi na hazitekelezwi.
11:53 Waangalizi wa Umoja wa Ulaya: Visa vya kukamatwa na kuhangaishwa kwa wapinzani viliripotiwa katika zaidi ya wilaya 20. Sana waathiriwa walikuwa wa chama cha FDC.
11:52 Waangalizi wa Umoja wa Ulaya : "Tume inakosa uwazi na wadau hawana imani nayo. Tume haina uwazi katika kufanya maamuzi na katika kuwafahamisha wapiga kura kwa wakati na kwa ufasaha."
11:50 Waangalizi wa Umoja wa Ulaya washutumu kukamatwa kwa mgombea urais wa chama cha FDC Dkt Kizza Besigye jana.
11:41 Matokeo ya uchaguzi wa urais ya karibuni zaidi: Vituo 23,308 kati ya jumla ya vituo 28,010, Rais Yoweri Museveni ana kura 5,047,754 (61.55%) naye Kizza Besigye 2,826,444 (34.47%). Vituo ambavyo matokeo yametangazwa ni asilimia 83.21 ya vituo vyote.
Matokeo kwa sasa (Vituo 23,308 kati ya 28,010)
Abed Bwanika75,9160.93%
Amama Mbabazi122,8481.50%
Baryamureeba Venasius46,8260.57%
Benon Biraaro22,2130.27%
Kizza Besigye2,826,64434.47%
Joseph Mabirizi21,6610.26%
Maureen Kyalya36,9400.45%
Yoweri Museveni5,047,75461.55%
Chanzo: Tume ya Uchaguzi Uganda (EC)
11:30 Magazeti mengi Uganda yameongoza na habari za mawaziri ambao wameshindwa kwenye uchaguzi wa ubunge.
Miongozi mwa walioshindwa ni:
  • Waziri wa Ulinzi - Crispus Kiyonga
  • Waziri wa Haki - Kahinda Otafiire
  • Waziri wa Habari - Jim Muhwezi
  • Waziri wa Elimu - Jessica Alupo
  • Mwanasheria Mkuu - Fred Ruhindi
Gazeti la New Vision limeongoza na kichwa cha kufafanua ni kwa nini mawaziri wakashindwa uchaguzini.

11:25 Waangalizi wa Umoja wa Afrika wakitaka kituo cha utangazaji cha taifa Uganda kutopendelea baadhi ya wagombea. Pia, polisi wasipendelee upande mmoja.
11:21 Kituo kikuu cha mabasi ya kuelekea miji mbalimbali Afrika Mashariki mjini Kampala kimebaki mahame huku matokeo kamili ya uchaguzi mkuu yakitarajiwa.
11:16 Maafisa wa jeshi wanashika doria katika barabara ya Entebbe mjini Kampala, huku polisi nao wakiendelea kushika doria makao makuu ya chama cha FDC cha Dkt Kizza Besigye.
11:10 Viongozi wa Tume ya Uchaguzi wameketi wakijiandaa kutoa mkumbo mwingine wa matokeo ya uchaguzi wa urais.
10:37 Kiongozi wa waangalizi wa IGAD Yufnalis Okubo asema kwa maoni ya kundi lake la waangalizi, uchaguzi ulitimiza viwango vinavyohitajika kimataifa. Ahimiza walioshiriki kukubali matokeo. Awataka wasioridhika kutumia mifumo ya sheria kulalamika.
10:30 Kiongozi wa waangalizi wa IGAD Yufnalis Okubo anasema kulikuwa na changamoto katika kuandaa vituokwa upigaji kura pamoja na kufunguliwa kwa vituo. Asema pia waliona mabango ya kampeni katika baadhi ya vituo vya kupigia kura. Asema siku ya uchaguzi, baadhi ya wapiga kura walikosa majina yao vituoni. Wasiojua kusoma hawakusaidia vyema. Waliofaa kupaka watu wino baada ya kupiga kura katika baadhi ya maeneo hawakumakinika sana. Apendekeza vifaa vya kupigia kura viwe vikifikishwa mkesha wa siku ya kupiga kura, sawa na kuandaliwa kwa vituo.
10:25 Kiongozi wa waangalizi wa COMESA Ashraf Gamaal Rashed amesema Tume ya Uchaguzi inafaa kuwezeshwa zaidi ili kutekeleza majukumu yake vyema.
10:20 Waangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, COMESA na IGAD wanatoa taarifa zao kuhusu uchaguzi. Rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi amewapongeza wananchi wa Uganda kwa kujitokeza kwa wingi. Amesema uchaguzi ulifiofanyika wiki hii ulikuwa na ushindani mkubwa.
09:59 Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umekanusha taarifa ambazo zimekuwa zikisambazwa mitandaoni zikiashiria kwamba Marekani imewaagiza raia wake waondoke Uganda. Ubalozi huo umesema taarifa hizo ni za uongo.
08:44 Bw Kiggundu amesema matokeo mengine yanatarajiwa mwendo wa saa nne, lakini yanaweza yakatangazwa mapema iwapo yatakuwa tayari. Ametetea tume hiyo dhidi ya madai kwamba kura kutoka 'ngome za upinzani' hayajaripotiwa. Tume inatarajiwa kutangaza matokeo kamili kabla ya saa kumi alasiri kwa mujibu wa sheria.
08:38 Matokeo yaliyotangazwa sasa hivi ni kama ifuatavyo. Ni kutoka vituo 21,254 kutoka kwa vituo 28,010. Matokeo yaliyotangazwa yanajumuisha kura 7,822,737 ambazo ni sawa na asilimia 51,21 ya wapiga kura 15 milioni waliosajiliwa na tume hiyo. Kumbuka si wapiga kura wote waliosajiliwa ambao hufanikiwa kupiga kura.
Matokeo kwa sasa (Vituo 21,254 kati ya 28,010)
Abed Bwanika70,7080.95%
Amama Mbabazi112,0711.50%
Baryamureeba Venasius42,9310.58%
Benon Biraaro20,5530.28%
Kizza Besigye2,603,88034.94%
Joseph Mabirizi19,6610.26%
Maureen Kyalya32,7730.44%
Yoweri Museveni4,549,14861.05%
Chanzo: Tume ya Uchaguzi Uganda (EC)
08:33 Mwenyekiti wa EC Badru Kiggundu anaanza kutangaza matokeo ya karibuni zaidi.
08:32 Kwa sasa ni wakati wa maombi Namboole, kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya kwanza ya urais ya karibuni zaidi leo.
08:28 Katibu Mkuu wa chama tawala cha NRM Justine Kasule Lumumba amekuwa akiwahutubia wanahabari kutoka Bweyogerere
Museveni anaongoza. NRM inaongoza katika kura za urais na za ubunge na tunasubiri matokeo ya mwisho. Hata kule mawaziri wameshindwa, ni watu wa kawaida. Waganda waliamua nani anafaa kuwaongoza. Kwa NRM si habari njema, lakini ni lazima tukubali.
08:13 Waangalizi wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kuhutubia wanahabari kuhusu uchaguzi mkuu wa Uganda saa sita kasorobo.
08:10 Mwenyekiti wa EC Badru Kiggundu ameingia ukumbini kutangaza matokeo ya karibuni zaidi ya uchaguzi.
07:54 Tume ya taifa ya uchaguzi Uganda inatarajiwa kutoa matokeo mengine mwendo wa saa mbili asubuhi.
07: 52 Matokeo yaliyotangazwa kufikia sasa ni kama ifuatavyo:
Matokeo kwa sasa (Vituo 15,799 kati ya 28,010)
Abed Bwanika51,150
Amama Mbabazi88,900
Baryamureeba Venasius33,135
Benon Biraaro15,588
Kizza Besigye1,767,041
Joseph Mabirizi14,757
Maureen Kyalya24,536
Yoweri Museveni3,156,070
Chanzo: Tume ya Uchaguzi Uganda (EC)
07:50 (Saa za Afrika Mashariki) Hujambo! Twatumai umeamka salama. Karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu uchaguzi mkuu wa Uganda. Matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi nchini Uganda yanaendelea kutangazwa, matokeo kamili yakitarajiwa kutolewa baadaye leo alasiri.

No comments:

Post a Comment