Trump alitwaa jimbo la South Carolina, Clinton ashinda Nevada.
Gavana wa zamani wa jimbo la Florida Jeb Bush amejiondoa kutoka kinyang'anyiro cha kugombea urais Marekani baada ya kushindwa vibaya katika uchaguzi wa mchujo wa vyama katika jimbo la South Carolina. Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump ameshinda katika uchaguzi huo wa mchujo katika jimbo hilo na hivyo kumuweka katika nafasi nzuri ya kuwa mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho cha Republican katika uchaguzi mkuu huku mgombea urais wa chama cha Democrats Hillary Clinton naye akimshinda Bernie Sanders katika jimbo la Nevada. Trump amemshinda kwa urahisi Seneta wa jimbo la Florida Marco Rubio na seneta wa Texas Ted Cruz. Huo ni ushindi wa pili mfululizo kwa Trump baada ya kuibuka mshindi pia katika jimbo la New Hampshire mnamo tarehe 9 mwezi huu. Marekani itafanya uchaguzi mkuu mwezi Novemba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment